Rais John Magufuli ametoa wito kwa wananchi kupuuza baadhi ya
viongozi wa kisiasa wanaotoa taarifa kuwa nchi inakabiliwa na tatizo la
njaa na badala yake wajikite kufanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeo
ya taifa.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara mjini Bariadi mkoani Simiyu
Rais Magufuli amesema taarifa hizo ni uzushi usiotakia mema nchi kwani
akiwa ni Rais wa Tanzania ndiye mwenye mamlaka ya kutoa taarifa za njaa
kwa mujibu wa sheria taratibu za nchi.
Rais Magufuli ambaye yuko ziarani mkoani Simiyu pamoja na mambo
mengine amezindua mradi wa ujenzi wa barabara ya lami yenye urefu nwa
kilometa 71.2 kutoka Lamadi hadi Bariadi huku barabara hiyo ikitajwa
kuwa na faida lukuki.
COMMENT AND SHARE...........!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!