Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli, yuko mjini
Addis Ababa nchini Ethiopia ambako anahudhuria mkutano wa 28 wa wakuu wa
nchi wanachama wa Jumuia ya Umoja wa Afrika (AU).
Hii ndiyo mara
ya kwanza ya Rais Magufuli anahudhuria mkutano huo tangu aingie madaraka
kuongoza Serikali ya Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Novemba mwaka 2015.
Akiwa Addis Ababa Rais Magufuli anatarajiwa
kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa Bara la Afrika
wanaohudhuria mkutano huo, mkutano ambao pia utahudhuriwa na Katibu Mkuu
wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.
Mkutano huo pia utatumiwa kumchagua mwenyekiti mpya wa tume ya Umoja wa Afrika (AU).
Wale
wanaowania wadhifa huo wa mwenyekiti ni pamoja na waziri wa mambo ya
nchi za kigeni wa Kenya Amina Mohammed, mwanadiplomasia Abdoulaye
Bathily kutoka Senegal, waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Chad
Moussa Faki Mahamat, mwanasiasa mkongwe kutoka Botswanda Pelonomi
Venson-Moitoi na aliyekuwa wakati mmoja mshauri wa rais wa Equatorial
Guinea Mba Mokuy.
COMMENT AND SHARE.....................!!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!