
Kuchukua namba kutoka kwa mwanamke ni rahisi zaidi kuliko hata kutamka
jina lako. Unachohitajika ni kuenda moja kwa moja kwa mwanamke unayetaka
kumuomba namba halafu unamwagiza akupatie. Mara nyingi mwanamke hawezi
kukataa kukupatia namba yake unless uwe umemuapproach kwa njia isiyofaa
ama hakujui. Mara ya mwisho mimi binafsi nilichukua namba kwa mwanamke chini ya
dakika moja ya kukutana na yeye. Nilikuwa nimeandamana na marafiki zangu
halafu mwanamke mmoja akapita kando yetu halafu muda wa dakika nikaamua
kumuaproach na kunipatia namba yake ya simu hapo hapo.
Kama bado unatatizika ni njia gani za kuchukua namba ya simu kutoka kwa
mwanamke basi fuata maagizo haya ya haraka ambayo nitakuelezea.
#1 Jiamini. Kujiamini ni kitu muhimu. Wakati unapoamua kuapproach
mwanamke lazima uwe unajiamini. Utajiamini vipi? Kujiamini ni rahisi.
Kile unachohitajika kufanya ni kuweka nia kuwa wakati ambapo
utamwaproach mwanamke lengwa basi lazima namba yake ya simu atakupatia.
Huko ndiko nikujiamini.
#2 Kuwa na mawazo chanya. Mawazo chanya ni mawazo ambayo
yanakubaliana na wewe. Mfano unaweza kuwa unataka kufanya kitu, halafu
katika akili yako umeweka dhana ya kuwa kile ambacho unakusudia kufanya
basi kitafanikiwa. Haya ndio tunayaita mawazo chanya. Ni dhana ambayo
unaamini kuwa itatokezea. Ukiweka mawazo chanya kuwa ukiapproach
mwanamke flani na atakupa namba yake ya simu basi bila shaka
utafanikiwa. Lakini ukiweka mawazo ya kuwa hautafanikiwa basi kweli
hautafanikiwa.
#3 Kuwa mwigo. Wakati mwingine inakuwa vigumu kabisa kwa wanaume
flani kuongea na mwanamke. Inakuwa vigumu zaidi kuomba namba kutoka kwa
mwanamke. Njia rahisi ya kutatua shida hii haraka ni kuigiza. Kuomba
mwanamke namba haichukui zaidi ya dakika mbili, hivyo unaweza kuwa
mwigo. Unaweza kuigiza vile rafiki yako anavyoomba namba ya simu ama
unaweza kufanya mazoezi kivyako kabla kumuapproach mwanamke kumuomba
namba ya simu.
#4 Relax. Wakati unapoach mwanamke lazima uwe umetulia. Punguza
wasiwasi, toa kijasho chochote ambacho uko nacho, pumua kiutulivu na
uondoe ubabaifu wowote ulio nao. Hii itakusaidia kwa kuwa ukiwa umerelax
utakuwa na nafasi nzuri ya kukumbuka mambo ambayo umeyapanga kumwambia
mwanamke flani. Hivyo ni muhimu kurelax kabla ya kuchukua approach
yeyote.
Njia nzuri ya kumuapproach mwanamke
Njia rahisi ya kuomba namba ya simu kutoka kwa mwanamke ambaye unamjua
na anakutambua ni ile ya moja kwa moja. Ukimwona anatembea mtaani halafu
wewe umesimama na marafiki zako, mwanzo hakikisha umefuata masharti
tuliyoyaeleza hapo juu; jiamini, relax, mawazo chanya na mwigo. Nenda
moja kwa moja na umwambie hivi:
"Mambo Mamito. Niko na ishu flani nataka kukuambia lakini sahizi
naona si wakati mzuri wa kukuambia... Nipatie namba yako ya simu
nitakupigia simu usiku."
ama
"Mambo Mamito. Napatie namba yako ya simu nataka kukupikia simu jioni nikwambie kitu flani"
Hii ndio njia ya moja kwa moja. Mwanamke wa kawaida, ambaye anakutambua
hawezi kukataa kukupatia namba yake ya simu. Mwanzo unaweza kuwa na
bahati ya kuwa huyu mwanamke alikuwa inteested na wewe tangu kitambo
lakini anashindwa jinsi angeweza kuwasiliana na wewe.
Kama ni mwanamke ambaye humjui na hakujui, basi ni vyema kwanza
ujitambulishe ili akufahamu. Si lazima uchukue namba yake ya simu siku
io hio bali unaweza kungojea muda mpaka mzoeane.
Wanaume wengi wanatatizwa na tatizo la kutojiamini na woga. Lakini
naamini kama unaweza kutatua mambo hayo mawili basi kazi yako itakuwa
rahisi.
COMMENT AND SHARE.............!!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!