MSANII wa muziki wa Bongo Fleva
Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ amejikuta akiishiwa pozi baada ya kupata
taarifa kuwa, msichana ambaye aliwahi kujianika kufanya mambo ya
usagaji, Malkia Said ‘Malkiz’ amemzimikia na yupo tayari kuolewa naye
hata mke wa nne.
Ishu hiyo ambayo ilizua viulizo ilijiri
siku chache zilizopita ambapo mwanadada huyo aliweka ujumbe huo kwenye
mtandao wa kijamii wa Instagram, akishikilia msimamo wake wa kuacha
usagaji na kudai kwa mara ya kwanza amejikuta akipagawishwa na Nuh japo
ni mume wa mtu.
Malkis alipoulizwa alisema; Pale
nilivyoandika nilisema nilikuwa nimelewa, lakini nikuhakikishie
sikukosea kuandika vile nikiwa kama binadamu mwenye hisia, niliona
niweke wazi hisia zangu, sijawahi kuvutiwa na mwanaume ila Nuhu natamani
hata anioe sababu dini yetu ya Kiislamu inaruhusu wake wanne na nipo
tayari kubadilika hata kimavazi.”
Nuh alipotafutwa kuhusiana na jambo hilo
alistaajabu na kujikuta akiangua kicheko mwanzo mwisho, kisha akaomba
shushushu wetu amuache kwanza kwa kuwa hakuwa na cha kujibu.
COMMENT AND SHARE................!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!