
Ni muhimu jamii ielimishwe umuhimu wa kupima afya zao na kuchukua hatua zinazostahili.
Jinsi ya kuzuia maambukizi ya VVU yanayotokana na kujamiiana
Kutokujamiiana kabisa (kugunga)
Kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu na asiye na uambukizo
Kujamiiana kwa kutumia kondomu ya kike au ya kiume kwa usahihi na wakati wote
Jinsi ya kuzuia maambukizi kwa mtoto mchanga
Wanawake wajawazito wahudhurie kliniki ili kupima na kufahamu afya zao.
Washauriwe vilevile wahudhurie na waume au wenzi wao ili kupata unasihi wa kupima VVU.
Wanawake wajawazito wanaobainika kuwa na VVU na wenzi wao wa kiume,
wapewe ushauri nasaha (unasihi) kuhusu uamuzi wa kunyonyesha au lishe
mbadala kwa mtoto mchanga
Wanawake wajawazito wanaobainika kuwa na VVU wapewe dawa za kuzuia
maambukizi kwa mtoto. Familia ambayo mama atakuwa amebainika kuwa na
virusi vya UKIMWI wakati wa ujauzito, ipewe rufaa ili kuendelea na
huduma au matibabu mengine kwa waishio na virusi vya UKIMWI.
Wanawake wote hasa wale waliobainika kuwa na VVU washauriwe kujifungulia
kwenye vituo vya afya. Wakina mama waliobainika kuwa na VVU ambao
wamejifungulia nyumbani wapeleke watoto kliniki ndani ya masaa 48 baada
ya kujifungua.
Jamii kwa ujumla ishirikishwe kutoa msaada wa hali na mali kuwawezesha
wakina mama walioambukizwa VVU kutimiza masharti ya kuzuia mambukizi
kwa mtoto.
Jinsi ya kuzuia maambukizo ya VVU wakati wa kutoa huduma
Ni muhimu watoa huduma wawe waangalifu wakati wa kuwahudumiawagonjwa na kuzingatia mambo yafuatayo:
Endapo mtoa huduma ana michubuko, majeraha au vidonda mikononi lazima
vifungwe vizuri kwa kitu kisichopitisha majimaji kama plasta au kuvaa
mipira ya mikononi wakati wa kumhudumia mgonjwa Kabla ya kugusa
nguo au vifaa vyenye damu, matapishi, mkojo au kinyesi cha mgonjwa ni
muhimu mtoa huduma kuvaa mipira ya mikononi na mgonjwa aelezwe sababu ya
kufanya hivyo.
Nguo au vifaa vyenye damu ya mgonjwa au majimaji mengine kutoka kwenye
vidonda viwekwe kwenye maji ya moto yanayochemka kwa dakika 20-30 au
vilowekwe kwenye JIC kwa dakika 20-30 kabla ya kufua/kuosha.
Mhudumu afue/asafishe vifaa hivyo akiwa amevaa mipira ya mikononi
Vitambaa vilivyofunga vidonda, mipira ya mkononi ilivyotumika kwa
kumhudumia mgonjwa wa UKIMWI viteketezwe kwa moto.Vifaa vingine
visivyochomeka vitumbukizwe katika choo cha shimo.
Mhudumu avae mipira ya mikononi wakati wa kumbeba mgonjwa mwenye vidonda.
Vifaa vyenye ncha kali vilivyotumika wakati kwa kumhudumia mgonjwa wa
UKIMWI na ambavyo vinaweza vikatumika tena vilowekwe kwenye JIC halafu
vichemshwe. Vile ambavyo havitatumika tena, vitumbukizwe kwenye choo
cha shimo.
Mhudumu aoshe mikono kwa sabuni kabla na mara baada ya kumhudumia mgonjwa.
COMMENT AND SHARE............................!!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!