Muhula mpya wa masomo sekondari na msingi kwa mwaka 2017 waanza Siku ya leo.:;
on
Get link
Facebook
X
Pinterest
Email
Other Apps
Wakati Muhula mpya wa masomo kwa mwaka 2017 kwa shule za msingi na
sekondari ukitarajiwa kuanza hii leo jumatatu katika mikoa mbalimbali
hapa nchini, siku ya jana idadi kubwa ya wazazi na walezi mkoani PWANI
waliendelea kufanya manunuzi ya vifaa mbalimbali vya shule
Wakati Muhula mpya wa masomo kwa mwaka 2017 kwa shule za msingi na
sekondari ukitarajiwa kuanza hii leo jumatatu katika mikoa mbalimbali
hapa nchini, siku ya jana idadi kubwa ya wazazi na walezi mkoani PWANI
waliendelea kufanya manunuzi ya vifaa mbalimbali vya shule ikiwa ni
pamoja na sare na madaftari.
Baadhi ya wazazi na walezi waliozungumza na TBC wamesema kuwa vifaa
vya shule kwa mwaka huu vimekua vikiuzwa kwa bei ya kawaida ambayo kila
mzazi ama mlezi anauwezo wakumudu bei hiyo.
Kwa upande wake Mbunge wa kibaha Vijijini AMOD JUMAA amekabidhi
shehena ya vitabu mbalimbali vya shule ya msingi na sekondari vyenye
thamani ya dola za kimarekani elfu 40 kwa ajili ya kupunguza tatizo la
upungufu wa vitabu katika shule mbalimbali mkoani PWANI.
Akipokea vitabu hivyo mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya
KIBAHA TATU SELEMANI amesema msaada huo utasaidia wanafunzi kupata
maarifa pamoja na kuwapunguzia waalimu adha ya kufundisha bila vitabu
COMMENT AND SHARE..................!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!