Baraza la Mitihani nchini – NECTA limetoa matokeo ya mitihani ya
upimaji kwa wanafunzi wa darasa la nne kwa shule zote za msingi nchini
pamoja na ule wa kidato cha pili kwa wanafunzi wa shule za sekondari
yanayoonesha ufaulu kuongezeka kwa 1.9%.
Katibu Mtendaji wa Baraza lza Mitihani
nchini Dkt Charles Msonde ndiye aliyetoa taarifa hiyo leo jijini Dar es
Salaam ambapo katika hali isiyo ya kawaida, shule tisa kati ya kumi
zilizofanya vibaya katika mtihani wa kidato cha pili nchini, zimetoka
mkoani Mtwara kama zinavyoonekana hapa
Amesema ufaulu umeongezeka kwa asilimia
1.9 kutoka 89.12% mwaka 2015 hadi kufikia 91.02% mwaka 2016 ambapo
wanafunzi 372,228 wamepata alama zinazowawezesha kuingia kidato cha tatu
huku wanafunzi 36,737 wakishindwa kufikisha alama hizo.
Shule ya St. Francis Girls ya Mbeya
imeongoza katika shule 10 bora kitaifa katika matokeo ya mtihani wa
kidato cha pili mwaka 2016
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, idadi ya
watahiniwa waliopata ufaulu mzuri wa madaraja ya I, II, na III ni
178,115 sawa na asilimia 43.55
Kuhusu ufaulu wa masomo, amesema, katika
masomo ya Civics, History, Geography, Kiswahili, Phiysics, Chemistry,
Chemistry, Biology na Basic Mathematics umepanda ikilinganishwa na mwaka
2015.
Aidha ufaulu kwa somo la English Language pekee ndio ambao umeshuka ikilinganishwa na mwaka 2015.
Somo lililofanyika vizuri zaidi ni
Kiswahili ambapo asilimia 90.06 ya wanafunzi wote, wamefaulu na soko
lenye ufaulu wa chini zaidi ni Basic Mathematics ambapo asilimia 21.55
wamefaulu.
Mwanafunzi aliyefanya vizuri zaidi ni
Teckla Erasmo Haule kutoka Canosa ya Dar es Salaam akifuatiwa na Joseph
Fabian Kalabwe wa Kwema Modern ya Shinyanga na Mirable Rayner Matowo wa
Canosa ya Dar es Salaam.
Katika wanafunzi 10 bora kitaifa, wanafunzi 9 ni wasichana, na watano kati yao wanatoka Feza Girls.
Matokeo ya wanafunzi 31 yamefutwa baada ya kubainika kuwa walifanya udanganyifu
COMMENT AND SHARE................!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!