Maafisa wa polisi nchini Zimbabwe
wamemkamata na kumzuilia mhubiri aliyetabiri kwamba Rais Robert Mugabe
atafariki mwezi Oktoba mwaka huu.
Pasta Patrick Mugadza alikamatwa
akiwa mahakamani mjini Harare Jumatatu ambapo alikuwa ameenda kwa kesi
nyingine dhidi yake, wakili wake Gift Mtisi ameambia wanahabari.
Alikuwa anakabiliwa na mashtaka ya kuvalia bendera ya taifa
"Alikuwa
amefika mahakamani kwa kesi hiyo polisi walipomkamata wakati wa
mapumziko na kumfungulia mashtaka kwa sababu ya unabii huo," Bw Mtisi
aliambia AFP.
"Awali alishtakiwa kwa kudunisha na kukosea heshima
mamlaka ya rais lakini shtaka hilo likabadilishwa baadaye na kuwa
kuwatusi watu wa asili fulani au dini fulani."
Pasta Mugadza,
ambaye huhudumu katika mji wa Kariba kaskazini mwa nchi hiyo, aliandaa
kikao na wanahabari wiki iliyopita ambapo alitabiri kwamba Mugabe
angefariki Oktoba 17 mwaka huu. Kumfanyia mzaha Rais Mugabe au kutoa unabii au ubashiri kumhusu ni jambo hatari nchini Zimbabwe.
Nchini humo kuna sheria ambayo huharamisha "kudunisha mamlaka ya au kumtusi rais."
Mwaka
2015, Mugadza alikamatwa na kuzuiliwa kwa karibu mwezi mmoja baada ya
kujitokeza hadharani na bango lililokuiwa na ujumbe uliomwambia Mugabe
kwamba watu wamekuwa wakiteseka chini ya utawala wake.
Siku ya
maadhimisho ya uhuru mwaka jana, alitoa mahubiri akiwa amejifungia
kwenye boriti ya taa nje ya duka kubwa zaidi la kibiashara mjini Harare,
akisema hiyo ilikuwa ishara ya raia kukandamizwa Zimbabwe.
Rais Mugabe amekuwa madarakani tangu 1980.
Kumekuwa na uvumi kuhusu afya yake na mara kwa mara husafiri mataifa ya Asia kwa matibabu.
Bw Mugabe amekataa kumtaja mrithi wake na chama chake cha ZANU-PF kimekuwa kikiyumbishwa na makundi ya watu wanaotaka kumrithi.
Mwishoni mwa mwaka uliopita, raia na wafuasi wa vyama vya upinzani waliandamana kupinga utawala wake.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!