Mapenzi ni hisia zisizozuilika na huwa hazichagui wakati, umri, rangi, dini, ama kabila; na ndio maana ikasemekana “penzi ni kikohozi kulificha huwezi”.
Asilimia kubwa ya wanaume wamekuwa wakilalamikia kuachwa na wapenzi ama
wake zao bila kufahamu nini wafanye ili kuweza kuzuia mambo haya.
Basi
usikonde wala usisononeke kwa sababu Kona ya Mahaba ipo kwa ajili yako
kukuweka sawa ili usiachike wala usikimbiwe na mpenzi wako.
MWONESHE/ MPE MAHABA
Wanaume
wengi wanashindwa kuwa wakarimu na wabembelezaji kwa wanawake zao,
waacheni waiite Tanga Mapenzi yalipozaliwa kwani ni ukweli usiopingika
wanaume wa Kitanga wanajitahidi kwenye ‘kupetipeti’.
MSILIKILIZE
Asilimia
kubwa ya wanawake wanapenda kusikilizwa na hii iwe ana haki au hana
haki jenga tabia ya kumpa nafasi ya kumsikiliza na kumshirikisha kwenye
maamuzi yako hii itamfanya ajione mwenye thamani kwako.
MRIDHISHE
Kwenye
tendo la ndoa hakikisha unamridhisha kadri ya uhitaji wake na
ikiwezekana mpaka mwenyewe akiri kuwa ameridhika, kama usipomridhisha
jiandae wenzio kukusaidia majukumu yako.
Ukiweza kuzingatia mambo
haya makuu matatu basi utakuwa umetii kiu ya mpenzi wako na kamwe hata
kukimbia kwa sababu msingi upo hapa, hayo mengine ni ziada tu.
COMMENT AND SHARE.....................!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!