Malkia wa Uingereza kwa mara
nyengine amekosa kuhudhuria ibada ya kuadhimisha mwaka mpya katika
kanisa la Sandringham kutokana na homa makali.
Malikia Elizabeth
pia alikosa ibada ya siku kuu ya Krismasi nyumbani kwake huko Norfolk
na hajaonekana hadharani kwa siku 12 sasa.
Msemaji wa Kasri la Buckingham amesema kuwa malkia anaendelea kupata nafuu.
Malkia wa Uingereza akosa ibada ya Krismasi
Yeye
na Duke wa Edinburgh walichelewa kwa likizo yao ya Krismasi kwa siku
moja mnamo Disemba 22, na kusafiri kwa kutumia ndege aina ya helikopta
badala ya treni kutokana na homa.
Mwanamfalme Phillip amepona.
Binti Mfalme Anne aliulizwa vile mamake alivyokuwa akiendelea alipowasili katika kanisa ambapo alijibu vyema.
COMMENT AND SHARE..........................!!!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!