Utangulizi:
Magonjwa ya ngono ni magonjwa yanayoambukiza kwa njia ya tendo la
kujamiiana na mtu aliyeambukizwa magonjwa hayo bila kutumia kondom.
Magonjwa haya huweza kuwa-pata watu wa rika na jinsi zote hususani wale
walio katika umri wa kuzaa (kati ya miaka 15-49).
Vijana wenye umri kati ya miaka 10 hadi 24 wanawakilisha moja ya tatu
(1/3) ya idadi ya wakazi wote wa Tanzania. Kundi hili liko katika
hatari zaidi ya maambukizi ya magon-jwa ya ngono kwa kuwa wanapobalehe
wanapata hisia za kupenda na pia hamu ya kufanya tendo la
kujamiiana hujitokeza kwa nguvu. Hali hii huchochewa na vichocheo
/homoni vilivyomo mwilini ambavyo katika kupanda na kushuka
husababisha hisia za kufanya tendo la kujamiiana. Hivyo basi, ikiwa
watakosa ufahamu wa kutosha kuhusu milli yao wanaweza kujiingiza
katika tabia hatarishi za kujamiiana bila kondomu na mwenzi zaidi ya
mmoja.
Aina za magonjwa ya ngono:
Kuna aina mbalimbali za magonjwa ya ngono ambayo yamegawanywa katika makundi kutokana na dalili zake kama ifuatavyo:
• Magonjwa yenye dalili za kutokwa na usaha au
majimaji sehemu za siri (ukeni na uumeni) ambayo ni Kisonono,Trikomonas na Kandida.
• Magonjwa yenye dalili za kutokwa na vidonda
ambayo ni Kaswende, Pangusa na Malengelenge sehemu za siri.
• Magonjwa yenye dalili za kutokwa na uvimbe
ambayo ni Mitoki, Pangusa na Malengelenge sehemu za siri.
Ieleweke kwamba, mtu anaweza kuwa na zaidi ya ugonjwa mmoja wa ngono kwa
wakati mmoja. Kujitokeza kwa dalili za ugonjwa wa ngono hutegemea aina
ya ugonjwa, jinsi na kinga ya mwili. Hata hivyo, baadhi ya watu
hawaonyeshi dalili yoyote. Asilimia 10-15 ya wanaume na asilimia 60-70
ya wanawake wenye kisonono hawaonyeshi dalili yoyote Hivyo basi, ni
muhimu kijana unapoelezwa na mwenzi wako uliyefanya nae tendo la
kujamiiana kwamba ameambukizwa ugonjwa wa ngono usisite kwenda kituo
cha huduma ya afya kwa uchunguzi na tiba hata kama huna dalili.
Dalili za magonjwa ya ngono:
Kijana uonapo dalili moja, au zaidi kati ya hizi zifuatazo nenda kwenye kituo cha huduma ya afya kwa uchunguzi;
Kwa kijana wa kike
• Maumivu chini ya kitovu
• Kutokwa na usaha au majimaji yenye harufu mbaya
sehemu za siri (angalia picha)
• Kuwashwa sehemu za siri
• Vidonda na vipele sehemu za siri, mdomoni na sehemu nyingine za mwili
• Maumivu wakati wa kujamiiana
• Kuvimba mitoki
• Kuota sundosundo sehemu za siri
• Kukojoa mara kwa mara kunakoambatana na muwasho au maumivu
Kwa kijana wa kiume:
• Maumivu makali sehemu za siri wakati wa kukojoa
• Kutokwa na usaha sehemu za siri
• Vidonda sehemu za siri (angalia picha) Vidonda sehemu za mdomoni (angalia picha) Kuvimba mitoki
• Kupata malengelenge
• Kuota sundosundo (warts) sehemu za siri
Baadhi ya tabia ambazo zinaweza kuchochea kupata maambukizi ya magonjwa ya ngono kwa urahisi zaidi:
• Kujamiiana bila kondomu-vijana wengi hukosa
ujasiri wa kusisitiza matumizi ya kondomu kwa kuhofia kuachwa na wenzi wao
• Kujihusisha na ukahaba
• Kujamiina na wapenzi wengi
• Kunyonyana sehemu za siri-kwa kuwa vimelea vya magonjwa ya ngono
vinapatikana kwenye majimaji ya sehemu za siri ni rahisi mtu mwenye
maambukizi ya magonjwa ya ngono kumwambukiza mwenzi
wakati wa kunyonyana.
• Kunyonyana ndimi (kula denda)-baadhi ya vimelea vya magonjwa ya ngono hupatikana mdomoni
(Kisonono, Kaswende naVirusi vya UKIMWI) hivyo
huambukiza kupitia kunyonyana ndimi ikiwa mmojawapo ana maambukizi.

• Woga wa vijana wa kike kuwashawishi vijana wa
kiume kutumia kondom wakati wa kujamiiana kwa sababu ya mfumo dume.
• Kushiriki katika shughuli mbalimbali zinazosababisha
kufanya ngono bila mpangilio, kwa mfano; makundi yanayoenda ufukweni,
kuangalia filamu za ngono au kushiriki kwenye ngoma za jadi zinazochezwa
usiku kucha, disko na matamasha
• Tamaa ya kupata pesa pamoja na vitu vya thamani
kama simu za mikononi, magari kutoka kwa watu mbalimbali
• Kuhusika na vitendo vya ubakaji
• Utumiaji wa madawa ya kulevya au pombe ambayo
husababisha kijana kukosa ufahamu na hivyo kufanya ngono isiyo salama.
KUMBUKA:
Kuwa mwangalifu wakati wote iIi usiweze kutumbukia kwenye tabia hizo. Ikibidi kujamiiana tumia kondomu kwa usahihi
Athari za magonjwa ya ngono:
Magonjwa ya ngono yasipotibiwa mapema na kwa usahihi huweza kuleta athari zifuatazo kwa mgonjwa;
Kwa kijana wa kike:
• Kuziba kwa mirija ya uzazi ambako kunasababisha
aidha mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi au ugumba
• Maambukizi katika mfuko wa uzazi
• Kupata Magonjwa katika viungo muhimu mwilini • • • Magonjwa ya moyo na mishipa ya damu
• Kansa ya kizazi
• Mabadiliko ya hedhi
• UKIMWI
Kwa kijana wa kiume :
• Maambukizi katika kokwa za mbegu za uzazi
• Kuziba mirija inayopitisha mbegu za uzazi na kuleta
utasa
• Kupata matatizo ya kukojoa kwa sababu ya kuziba
njia ya mkojo.
• Kupata Magonjwa katika viungo muhimu mwilini
kama ubongo, moyo, na figo
• Magonjwa ya moyo na mishipa ya damu.
• Kansa ya uume
• Kupungua nguvu za kiume
• UKIMWI
KUMBUKA:
Athari zote hizi zinaweza kuepukika iwapo magonjwa ya ngono yatatibiwa
mapema na kwa usahihi. Usiogope! Magonjwa ya ngono yanatibika
Mbinu za kupambana na Magonjwa ya ngono kwa vijana:
Ili kuepukana na maambukizi ya magonjwa ya ngono zingatia yafuatayo:
• Usifanye kitendo cha ngono kabisa
• Jiepushe kufanya tendo la kujamiiana katika umri
mdogo
• Jiepushe na ulevi na madawa ya kulevya
• Jiepushe na vitendo vya ubakaji
• Jihadhari na kupiga denda na mwenzi usiyejua hall
yake ya afya
• Jiepushe na vitendo vya kunyonya uume au uke wa
mwenza
• Tumia muda wako mwingi katika masomo, kazi za
mikono, michezo na sanaa
• Epuka vishawishi kama zawadi na lifti za magari
barabarani
• Epuka kukaa na mpenzi wako peke yenu hasa
nyakati za usiku
• Epuka makundi ya vijana walevi, wazururaji na
wavuta bangi au watumiaji wa madawa ya kulevya
• Ikiwa umeoa au kuolewa, kuwa mwaminifu kwa
mwezi wako katika tendo la kujamiiana.
Kinga dhidi ya Magonjwa ya Ngono
• Acha ngono kabisa katika umri mdogo
• Tumia kondomu ya kike au ya kiume kwa usahihi
kwa kila tendo la kujamiiana
Mambo muhimu ya kuzingatia ukipata maambukizi ya magonjwa ya ngono:
• Wahi kwenye kituo cha huduma ya afya kilicho
karibu nawe kwa uchunguzi na matibabu sahihi
• Tumia dawa zote kwa kufuata maelekezo ya
mtaalam wa afya hata kama dalili za ugonjwa zimepotea
• Epuka kujinunulia dawa bila maelekezo ya mtaalam
wa afya
• Usifanye tendo la ngono mpaka utibiwe na kupona
kabisa
• Muarifu mwenzi wako mapema iii wote mkapate
matibabu sahihi na ushauri nasaha
KUMBUKA:
Kuwepo kwa magonjwa ya ngono kunaongeza uwezekano wa kuambukizwaVirusiVya UKIMWI .
Source Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI (NACP) S.L.P 11857, Dar es salaam, Simu: 2131213
Faksi: 2119833,Tovuti: www.nacp.go.tz
COMMENT AND SHARE.................!!!!!!!!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!