Kampuni ya kuunda magari ya Ford Afrika Kusini, yarejesha magari aina ya Kugas kwa sababu ya kuwaka moto
Kampuni
kubwa ya kuunda magari ya Ford imeanza kurejesha magari 4,500 aina ya
Kuga nchini Afrika Kusini kwa sababu ya kiusalama, baada ya zaidi ya
magari 50 kushika moto tangu mwaka 2015.
Mkurugenzi mkuu wa Ford,
Afrika Kusini Jeff Nemeth amesema kuwa uchunguzi unaonyesha kuwa kutokea
kwa moto, kulisababishwa na muongezeko wa joto kwenye injini yake na
kusababisha kuvuja kwa mafuta.
Bwana Nemeth alisema hayo katika
mkutano wa pamoja na waandishi wa habari kwa pamoja na tume ya wamiliki
na waundaji bidhaa ya Taifa hilo- NCC, ambayo imekuwa ikishinikiza
kampuni hiyo ya magari kuchukua hatua. "Swala hili limejikokota kwa muda
mrefu," amesema kamishena mkuu wa tume hiyo Ibrahim Mohammad.
Magari yanayorejeshwa ni yenye muundo wa uwezo wa kubeba mafuta lita 1.6 iliyojengewa Uhispania kati ya mwaka 2012 na 2014.
Kampuni
hiyo imo kwenye shinikizo kubwa kuchukua hatua tangu mwendesha gari
mmoja Reshell Jimmy, 33, alipoteketea hadi kufa ndani ya gari muundo wa
Kuga mwaka 2015.
Jumla ya magari 48 yameteketea nchini Afrika
Kusini, 11 kati yao mwezi huu pekee. Hayo yameripotiwa na gazeti moja la
nchi hiyo TimesLive.
COMMENT AND SHARE.......................!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!