
Rapper na mwanazuoni Nikki wa Pili, amefunguka kwa kudai kuwa label
kubwa kutoka ugaibuni zinakuja Afrika kusaini wasanii kwa lengo la
kuwanyonya na baadae kuwapoteza kwenye ramani ya muziki.
Rapper huyo wa Kundi la Weusi amezifananisha label hizo na makampuni ya
madini kutoka Ulaya ambayo amedai mara nyingi yakuja nchi za Afrika
kwaajili ya kupora rasilimali.
.
. “Ujio wa makampuni makubwa ya muziki Africa toka ugaibuni, hauna
tofauti na makampuni ya madini, lengo ni lile lile uporaji..time will
tell,” alitweet Nikki wa Pili.
Aliongeza kupitia Instagram kwa kusema, “Afrika Kusini na Nigeria muziki
wao wameukuza na kuutangaza wenyewe, toka enzi za P Square mpaka
Wizkid, au toka Marium Makeba mpaka Mafikizolo. Ujio wa wageni ndiyo
unakuja kuushusha. Mtazame #Davido toka amesainiwa na Sony na kabla ya
hapo au #Keko wa Uganda, au #RoseMhando. Hawa walisainiwa Sony na pili
makampuni hayo lengo ni kufungua milango ya huku kwa muziki wa nje ndiyo
maana Mtv Awards main artist alikuwa Future”
Hapa nchini Tanzania kwa sasa ni @officialalikiba pekee ndiyo ambaye yupo chini kampuni ya Sony.
UNAONAJE...!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!