Baada
ya wanaume kusifika kuwa ndio walaji wakubwa wa minofu ya samaki aina
ya Pweza na supu yake, hali sasa imebadilika baada ya kinadada kuonekana
pia wakichangamkia kwa wingi kitoweo hicho kinachotajwa kuwa na sifa za
kipekee kwa mujibu wa watumiaji.Inaelezwa
kwa wastani kupitia wauzaji waliozungumza na Nipashe imebainika kuwa
kuna ongezeko la takribani asilimia 40 ya wateja wanawake anbayo ni
karibu kila kwenye wateja 10 wanaoununua vipande vya Pweza au supu yake
kuwa wanne ni wanawake.Wanaume
ndiyo walikuwa wakisifika kwa ulaji wa supu ya Pweza uliopamba moto
jijini Dar es salaam katika miaka ya hivi karibuni kutokana na kuwepo
taarifa kwamba husaidia mambo mengi mwilini hasa katika kuimarisha
urijali kwa wanaume.UTAFITI WA KITABIBU:Dr.
Damas Mahenda ambaye ni Mhadhiri Msaidizi kutoka Chuo Kikuu cha Afya na
Sayansi Shirikishi (MUHAS) amesema ni kweli samaki jamii ya Pweza
wanafaida nyingi mwili hivyo si ajabu kusikia watu wakichangamkia
matumizi yake wakiwemo akina mama.Dr.
Mahenda amesema Pweza wamejawa na virutubisho vinavyosaidia mengi
ikiwemo kuongeza hamu na kuboresha tendo la ndoa huku minofu yake ikiwa
virutubishpo vya kumuwezesha mwanamke kuwa na sifa halisi za “Ukike” na
pia mwanaume kuimarika afya yake.
COMMENT AND SHARE.................!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!