
Rapper wa kundi la Weusi, Joh Makini amefunguka sababu ya kuchelewa kwa wimbo wao na Sauti Sol kutoka Kenya.
Mwezi Septemba mwaka jana, Joh alithibitisha kupitia mtandao wa
Instagram kuwa wimbo huo ungetoka kabla mwaka huo haujaisha lakini mpaka
sasa bado haujatoka.
Akiongea na Bongo5, Joh amesema sababu ya kuchelewa kutoka kwa wimbo huo
ni kutokana na baadhi ya marekebisho yaliyokuwa yanatakiwa kufanyika
katika wimbo huo ambapo wote kwa pamoja walikuwa busy na kazi nyingine.
“Sauti Sol kama ambavyo unawafuatilia utagundua ni watu ambao wako busy
sana na sisi pia hivyo hivyo. Ngoma tulishaifanya lakini kama wasanii
pia tuligundua kuna vitu turekebishe. Hiyo ndio sababu kubwa na sasa ipo
tayari,” amesema Joh.
“Mipango ya video ikiwa tayari na vile ambavyo sote tutakua tayari
itoke. I mean sisi na Sauti Sol ili tuweze kupromote kwa pamoja isiwe
kwa upande mmoja,” ameongeza.
COMMENT AND SHARE............!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!