Kuna vitu vingi ambavyo unaweza kutumia kwa manufaa yako ili kufanya
wanawake wakuone unavutia. Amini usiamini, hivi vitu si lazima uwe
tajiri wala uwe na urembo wowote. Mwanzo kati ya vitu hivyo vingi ni
rahisi kuvitumia kwa urahisi. Hii hapa ni orodha ya mambo ambayo
ukiyazingatia yatakufanya wewe uwe na mnato kwa mwanamke yeyote yule.
1. Uwezo wako wa nishati
Nishati inaweza kuwa na mkusanyiko wa
vitu kadhaa, kama vile kuhisi kwa vipepeo ndani ya tumbo, kusuka,
wasiwasi ama vitu tofauti kabisa. Kwa mtizamo wa moja kwa moja, nishati
inahusiana na yote yale ambayo yanamfanya mwanamke kujiskia raha wakati
anapokuona ama kutaka kuutumia muda wake mwingi akiwa na wewe. Nishati
inacheza nafasi kubwa katika mapenzi kama wataka kumtongoza mwanamke na
ufaulu kwa urahisi. Ili kupeana nishati zaidi kila wakati unapokuwa na
mwanamke, hakikisha kile kikuu unachohitaji kufanya ni kumchekesha,
kumsapraiz, umguse kwa bahati mbaya mara kwa mara, kuwa mwenye michezo
nk. Zote hizo zitamfanya kukufikiria wewe mara 24/7.
2. Mbinu utakayoitumia kumsifu
Kulingana na utafiti kutoka NBC
unadai ya kwamba wanawake wengi hawajiskii huru kupewa ama kupokea sifa
kutoka kwa wanaume. Lakini usikatwe na tamaa! Vile ambavyo utampongeza
mwanamke inaweza kucheza pakubwa kufaulu kumpata mwanamke unayempendae
baada ya muda. Afterall ukimsifu kitofauti tofauti anaweza kukubali ama
kukuona kama wewe ni mzaha kwake. So kuhepa aibu kama hizi ndogo ndogo,
unafaa umsifu mwanamke kwa jambo ambalo ni la kwake pekee, yaani kitu
ambacho utamsifu nacho hakipatikani kwa mwingine. Mfano waweza
kumakinika kwa kitu ambacho anafanya wakati flani na utumie ujuzi wako
wa kiume kumsifia na jambo hilo. Mfano unaweza kumsifu kwa uwezo wake wa
kuimba, kuchora, mtindo wake wa kutembea nk. [Soma: Mbinu ya kutongoza
kwa wale wanaojifunza]
3. Upambo wako
Si lazima uwe mwanamume wa kuvutia ili umvutie
mwanamke. Utafiti umebainisha kuwa wanawake hawavutiwi na urembo wa
mwanamume, nywele zake wala ngozi yake. Mwanzo kuwa mrembo kama
mwanamume kuna ubaya wake mwingi ikizingatiwa kuwa unaweza kuonekana
kama pleya ambaye unapendwa na wanawake wengi.
Kile ambacho unachohitajika hapa ni uhakikishe kuwa uwe nadhifu
kimwili na mavazi yako. Kufanya hivi kutakusaidia wewe kuonekana mtu
timamu halikadhalika inakufanya wewe kuwa na confidence ya kapproach
demu yeyote yule.
4. Ujuzi wako wa kutangamana
Lazima atleast uwe na ujuzi ambao
utakusaidia wewe kuweza kutangamana na wengine. Kama mwanamume lazima
uwe na ujuzi ambao utakusaidia wewe kutangamana na wengine kwa urahisi.
Hii inamaanisha kuwa lazima uwe na ujuzi flani wa kuongea na wanawake
ndipo utakapojua jinsi ya kumfanya apagawe na wewe.
5. Kiwango chako cha kujiamini
Kitu cha mwisho ambacho ni muhimu
kwako kuwa nacho ni kujiamini. Kujiamini ni njia moja wapo ya lazima uwe
nayo ili uweze kuiteka hisia ya mwanamke yeyote yule.[Soma: Njia za
kuwa na confidence kama mwanaume]
KUMBUKA: Vitu vyote tulivyoeleza hapo juu havitakuwa na manufaa
yeyote yale iwapo kama hutaweza kujiamini kama mwanamume. Hivyo ni
lazima kwako kuhakikisha kuwa mwanzo unajijenga kwa kuwa na confidence.
Hii ni kuanzia kujitambua wewe mwenyewe bila kujishuku, kuongea bila
woga wowote wala kutoingiwa na wasiwasi wakati wowote ukiwa karibu na
mwanamke.
COMMENT AND SHARE...................!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!