Mshindi wa uchaguzi mkuu wa mwezi
Novemba Donald Trump anatarajiwa kuapishwa kuwa rais wa 45 wa Marekani
Ijumaa tarehe 20 Januari, 2017.
Bw Trump wa chama cha Republican
anatarajiwa kuapishwa mbele ya watu 750,000 mbele ya majengo makuu ya
bunge la Marekani, Capitol Building, Washington D.C.
Kisheria, rais anafaa kuapishwa kabla ya saa sita mchana saa za Amerika Mashariki ambazo Afrika Mashariki ni saa mbili usiku.
Hii hapa ni ratiba fupi ya matukio yanayotarajiwa siku hiyo.
Saa 17:30 (Saa za Afrika Mashariki) Wanamuziki walioalikwa wataanza kutumbuiza.
19:30 Hotuba za kufungua sherehe zitaanza kutolewa.
20:00
Muda mfupi kabla ya saa Mbili Afrika Mashariki Donald Trump atalishwa
kiapo cha kuwa rais wa Marekani na Jaji wa Mahakama ya Juu John Roberts.
Baadaye,
kutakuwa na msafara baada ya sherehe ya kuapishwa ambao utaanza katika
vidato vya jumba la Capitol Building kuelekea ikulu ya White House
kupitia barabara maarufu ya Pennsylvania Avenue.
Bw Trump na mkewe
Melania baadaye watacheza densi katika matamasha matatu, mawili katika
ukumbi wa mikutano wa Walter E Washington na jingine katika ukumbi wa
Jengo la Makumbusho ya Taifa. Miaka minane iliyopita, Rais Obama alipokuwa anaapishwa kura rais, waliohudhuria walikuwa 1.8 milioni.
Siku moja baada ya kuapishwa kwa Bw Trump, wanawake takriban 200,000
wanatarajiwa kuandamana Washington DC na miji mingine kumpinga Bw Donald
Trump.
Hillary Clinton na mumewe Bill wamethibitisha kwamba watahudhuria sherehe hiyo, sawa na George W Bush na mkewe Laura.
Wamesema wanataka "kushuhudia kukabidhiwa madaraka kwa rasi mwingine kwa njia ya amani."
Rais
mwingine wa zamani Jimmy Carter atahudhuria pia, lakini George HW Bush,
92, na mkewe Barbara hawataweza kwa sababu za kiafya.
COMMENT AND SHARE...................!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!