Inadaiwa Arsenal wapo kwenye mazungumzo yaliyochangamka na meneja mpya kuchukua nafasi ya Arsene Wenger msimu ujao
Bosi huyo wa Kifaransa amekuwa akiinoa Arsenal
kwa muda wa zaidi ya miaka 20 sasa, na amewaongoza katika nyakati ngumu
za uchumi huku akiwahakikishia nafasi yao katika michuano ya Ulaya.
Wenger kwa umaarufu ameiongoza timu yake, ikimaliza msimu bila
kufungwa hata mechi moja katika msimu wa 2003-01 Ligi kuu, lakini licha
ya hatua hiyo, amekuwa akishambuliwa na mashabiki wanaotaka mafanikio
miaka ya hivi karibuni.
Makundi hayo ya mashabiki yamejaribu kupinga yakitaka mabadiliko
katika klabu hiyo, wakati mabango yakimtaka Mfaransa huyo kuachia ngazi
yalionekana kuzagaa katika uwanja wa Emirates.
Mkataba wa Wenger unakaribia kufika mwisho msimu ujao wa majira ya
joto, na kukiwa hakuna dalili ya mkataba mpya, klabu inafanya mchakato
wa kutafuta kocha mpya.
Massimiliano Allegri kwa sasa anadaiwa kuwa kwenye mazungumzo
yaliyochangamka na uongozi wa klabu kuchukua dili la kuinoa Arsenal.

Muitaliano huyo ametwaa taji la Ligi ya Italia akiwa na Juventus
katika misimu mitatu tangu alipochukua mikoba ya bosi wa sasa wa Chelsea
Antonio Conte aliyeondoka klabuni hapo kuinoa timu ya taifa ya Italia.
Bosi huyo wa Juve inaaminika kuwa anatamani sana kutua Uingereza
kushindana na Muitaliano mwenzake lakini makubaliano kwa ajili ya
kibarua kipya hayajafikiwa.
Meneja wa Leipzig Ralph Hasenhuttl na kocha wa Bournemouth Eddie Howe pia ni waalimu wanaopewa nafasi kubwa kumrithi Wenger.
Je! Allegri ni mtu sahihi kurithi nafasi ya Wenger?
COMMENT AND SHARE..............!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!