
Msanii wa muziki wa bongo fleva Lady Jaydee amefunguka na kusema
wanawake wengi wanaogopa kuanza maisha mapya ya mahusiano kwani wengi
wao wanashindwa kuondoka kwenye ndoa zao ambazo hazina afya.
Lady
Jaydee alisema hayo kupitia kipindi cha Wanawake Live kinachorushwa na
EATV na kusema wanawake wengi wanashindwa kufanya maamuzi kwa sababu
hawajiamini na wanaogopa kwenda kuanza maisha mapya.
"Wanawake wengi wanashindwa kutoka
kwenye mahusiano kwenye ndoa zisizo na afya ni kutokana na wao
kutojiamini, kwanza si jambo rahisi sana kama umekaa na mtu muda mrefu
harafu uamue tu kuwa unaondoka, ni kwamba kuna maisha ambayo mmejenga
pamoja kwa hiyo unapoondoka unakwenda kuanza maisha mapya, watu wengi
lile suala la kwenda kuanza maisha mapya ndiyo huwa wanaliogopa" alisema
Lady Jaydee.
Mbali na hilo Lady Jaydee anadai licha
ya watu wengi kuogopa kuanza maisha mapya lakini yeye aliamua kufanya
maamuzi ya kusonga mbele kwani hakuhitaji kubaki kwenye mahusiano ambayo
kwake yalikuwa hayana faida yoyote.
COMMENT AND SHARE....................!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!