Serikali ya Uganda, imethibitisha kuwepo kwa ugonjwa wa homa ya ndege katika maeneo karibu na fuo za Ziwa Victoria.
Virusi hivyo vimethibitishwa kwa ndege wanaohama, bata wanaofugwa na kuku.
Wakuu
sasa wametoa tahadhari kwa jamii za maeneo hayo kuhakikisha kuwa
ugonjwa huo hausambai na kuwaambukiza watu. Mwaandishi wa BBC nchini
Uganda, Catherine Byaruhanga. Anasema kuwa ripoti za awali za ndege
waliokufa zilianza kutolewa mwanzo tu wa mwaka huu.
Jamii za
maeneo hayo, wamesema kuwa, walizipata mizoga ya ndege wengi waliokuwa
wakihamia Uganda wakati wa majira ya baridi katika maeneo ya kaskazini
mwa dunia.
Majaribio kadhaa yaliyofanywa na wataalamu,
yalithibitisha kuwa, ndege hao walifariki kutokana na maradhi ya Highly
Pathogenic Avian Influenza au bird flu, yaani homa kali ya ndege kama
inavyofahamika.
Chembechembe zilizokusanywa kutoka kwa mizoga ya
bata wa kufugwa na kuku, katika Wilaya moja ya eneo hilo karibu na Ziwa
Victoria upande wa Uganda, zilithibitisha hilo.
Hakuna taarifa
zozote za ugonjwa huo kuambukiza binadamu, na serikali ya Uganda imesema
kuwa, inawashauri jamii za maeneo hayo kuhusu namna ya kujikinga
kupatwa na ugonjwa huo na mbinu za kuzua kuzambaa zaidi.
Vikosi vya majanga ya dharura vimetumwa huko ili kukusanya mizoga ya ndege hao waliokufa.
Hii
ni mara ya kwanza kwa mlipuko wa ugonjwa huo kutokea nchini Uganda,
lakini mamlaka kuu ya nchi hiyo, imefumbua mbinu mpya ya kukabiliana kwa
haraka namna ya kushughulikia majanga ya dharura ya kiafya, hasa
kufuatia visa vya ugonjwa hatari wa Ebola.
COMMENT AND SHARE.................!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!