Hawa Ndiyo Vijana 5 wa Sasa Wanaotikisa kwa Mkwanja Duniani.:;
on
Get link
Facebook
X
Pinterest
Email
Other Apps
Bado
kuna watu hawaamini kama mtu anaweza kuwa bilionea akiwa na miaka
midogo. Wanachokiamini ni kwamba ili uwe bilionea, ni lazima ujanani
upambane sana na mafanikio yanakuja kupatikana ukiwa na miaka hamsini,
ndugu yangu, kama ulikuwa ukifikiri hivyo, umekosea sana.
Kuna
vijana wanatengeneza pesa kwa sasa, wana umri mdogo lakini akaunti zao
benki zimenona ile mbaya. Achana na mabilionea wenye umri mkubwa kama
Bill Gates, Carlos Slim na wengineo, hebu cheki mabilionea vijana ambao
wanaogelea katika mabwawa yaliyojaa pesa. Evan Spiegel
Huyu
jamaa ni Mmarekani, ana umri wa miaka 25 tu. Ni Mmarekani aliyezaliwa
Los Angeles, California huko nchini Marekani. Mara baada ya kusoma
katika Shule ya Crossroads, akamalizia elimu yake katika Chuo cha
Stanford kilichokuwa hukohuko nchini Marekani.
Baada
ya kuona mitandao ya kijamii ikishika kasi, akamuita mshikaji wake,
Bobby Murphy na kumpa wazo la kutengeneza mtandao wa kijamii, wazo hilo
likaonekana kufaa hivyo kutengeneza Mtandao wa Kijamii wa Snapchat ambao
umekuwa maarufu kwa sasa.
Mpaka
sasa, mtandao huo umempa jamaa utajiri dola bilioni 2.1 (zaidi ya
trilioni 5.2) na kumfanya kuwa kijana mdogo mwenye pesa nyingi. Boby Murphy
Huyu
Jamaa ni Mmarekani mwenye asili ya Ufilipino mwenye umri wa miaka 27.
Alisoma katika Shule ya Madeleine iliyokuwa Calfornia nchini Marekani.
Baada ya kuona anajua sana hesabu, akaomba kujiunga na Chuo cha Stanford
ambapo huko ndipo alipokutana na mshikaji wake, Spiegel na kuamua
kutengeneza Mtandao wa Kijamii wa Snapchat ambao ulimuingizia fedha
nyingi tu.
Leo
unapomzungumzia Murphy, ni miongoni mwa mabilionea wadogo ambapo
anamiliki mkwanja wa dola bilioni 1.8 ambazo ni zaidi ya shilingi
trilioni 3.5.
Mark Zuckerberg
Wengi
wanamjua, na kama humjui basi bila shaka utakuwa ukitumia mitandao yake
ya Facebook, Instagram au WhatsApp. Mshikaji ana miaka 31, alizaliwa
huko White Plans, New York nchini Marekani. Alipokua, jamaa alisomea
katika Shule ya Ardsley, baadaye akaenda katika Akademi ya Phillip
Exteter na kumalizia katika Chuo Kikuu cha Harvard hukohuko Marekani.
Alipofika
hapo, akaamua kuanzisha Mtandao wa Kijamii wa Facebook kwa kuamini
kwamba ungempa pesa ndefu. Alifanikiwa, mtandao ukapata watumiaji wengi,
akanogewa, akanunua mitandao mingine ya WhatsApp na Instagram ambayo
mpaka leo inamuingizia fedha na kumfanya bilionea wa tano duniani huku
akiwa na utajiri wa dola bilioni 50 ambazo ni zaidi ya shilingi trilioni
100.
Dustin Moskovitz
Wakati
Mark Zuckerberg alipopata wazo la kuanzisha Mtandao wa Facebook, ndani
ya chumba alikuwa na watu wengine watatu. Mmoja wa watu hao ni huyu
jamaa ambaye alizaliwa Gainesvile, Florida hukohuko nchini Marekani
japokuwa baba yake ni Muisrael.
Mwaka
2008 jamaa akaamua kujitoa katika Kampuni ya Facebook na hivyo
kuanzisha programu yake ya Asana akiwa pamoja na rafiki yake ambaye naye
alikuwa akifanya kazi Facebook, Justin Rusenstein. Hapo, jamaa akaanza
kupata mafanikio mpaka kuwa na utajiri wa dola bilioni 20 ambazo ni
zaidi ya shilingi trilioni 40. Kwa sasa jamaa ana miaka 31.
Elizabeth Holmes
Ni
mwanadada mrembo, anayewavutia wanaume wengi. Ni mdogo, ana miaka 31.
Katika maisha yake, Holmes alisoma masuala ya utabibu katika Chuo cha
Stanford kilichokuwa nchini Marekani. Mwaka 2003 alipokuwa na miaka 19,
akagundua kifaa kinachoitwa Fingestick (kifaa maalumu kidogo
kinachotumika kuangalia wingi wa damu na magonjwa mbalimbali ya damu)
ambacho kiliweza kumpatia kiasi cha dola milioni 400 (zaidi ya bilioni
800) kwa mwaka wa kwanza tu.
Amekuwa
akiishi katika ulimwengu wa mabilionea, aliendelea kuingiza fedha kila
siku, akaunti yake kusoma dola milioni 30 zimeingia ni kitu cha kawaida
sana. Mpaka sasa, mrembo huyu ana utajiri wa dola bilioni 4.8 ambazo ni
zaidi ya shilingi trilioni 9.5. COMMENT AND SHARE...........................!!!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!