Meneja wa Manchester City Pep
Guardiola amesema kuwa timu yake kwa sasa inaweza kuondoka katika zile
timu zinazowania ubingwa baada ya kupokea kichapo cha 4-0 kutoka kwa
Everton.
Kwa sasa City wapo nyuma kwa alama 10 dhidi ya vinara Chelsea wenye alama 52.
Alipoulizwa kama alama 10 ni nyingi sana alijibu ndio sio rahisi kuzifikia.
Guardiola, mwenye miaka 45, amewaambia wachezaji wake kuungana wakati
huu wa kipindi kigumu na kutoangalia msimamo wa ligi mpaka mwisho wa
msimu.
''Mwishoni mwa msimu tutajitathimini kiwango chetu,ufundishaji ulikuwaje na wachezaji walikuwaje.
Baada ya hapo tutaamua kwa pamoja. Meneja huyo wa zamani wa Barcelona na Bayern Munich amesema kuwa ana
furaha sana kuwa ndani ya Manchester licha ya timu yake kuwa nafasi ya
tano.
COMMENT AND SHARE.....................!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!