
Elimu ya uzazi wa mpango bado haijawafikia vijana wengi sana hasa tanzania, wengi wao hudhani labda
matumizi ya dawa na njia za uzazi wa mpango ni kwa ajili ya malaya, watu
waliokwisha zaa na kadhalika. lakini hii sio kweli kwani njia hizi ni
nzuri kwa rika zote yaani vijana na watu wazima ambao wanashiriki ngono
ila kwa sasa hawako tayari kupata mtoto.
kutotumika kwa njia hizi kumesababishwa kuzaliwa kwa watoto wengi ambao
hawakupangwa, kujiua kwa wasichana kwa kukwepa aibu na utoaji wa mimba
wa mara kwa mara.
utafiti nilioufanya mwenyewe nimegundua kwamba msichana akiingia kwenye
mahusiano kwa miaka mitatu bila kutumia njia yeyote ya uzazi wa mpango
anaweza kutoa mimba nne mpaka tano lakini pia asilimia kubwa ya wanachuo
wa tanzania ambao huingia kwenye mahusiano vyuoni hawawezi kumaliza
chuo bila kutoa mimba hata moja.
kuna njia nyingi sana za uzazi wa mpango ikiwemo vitanzi, vijiti,
kondomu,kutumia kalenda, sindano,vidonge, upasuaji wa kufunga mirija na
kadhalika. kondomu ni njia bora sana kwani huzuia ukimwi na mimba pia
lakini ukweli ni kwmba kama kondomu zingekua zinatumika vizuri basi hao
watoto tusingewaona mtaani hivyo kama wewe hauko tayari kuzaa sasa hivi
kwa sababu yeyote ile nakushauri utumie njia ya kijiti.
njia hii ikoje?
kijiti cha plastiki chenye homoni za uzazi huwekwa kwenye mkono wa
mwanamke, homoni ndani ya kijiti hicho huzuia mimba kwa kwa kuzuia yai
kutoka kwenye kiwanda yaani ovari kwenda kwenye kizazi . kijiti hiki
huwekwa bure kwenye hospitali zote za serikali tanzania.
kwanini njia hii ni bora kuliko zote?
hurudisha uwezo wa kuzaa haraka: kama unatumia kijiti hata kama
kiliwekwa wiki iliyopita, ukibadilisha mawazo ukataka mtoto kinatolewa
na mwezi huohuo unapata mtoto, tofauti na njia ya sindano ambayo
ukichomwa leo kuna uwezekano wa kukaa mpaka miaka miwili bila kupata
mtoto.
ni rahisi kutumia: kijiti hiki kikishawekwa hospitali huhitaji
kukumbuka chochote tofauti na vidonge ambavyo wakati mwingine mtu huweza
kusahau asimeze akajikuta amebeba mimba.
inafanya kazi kwa muda mrefu sana; kama wewe ni binti mdogo au
wewe ni mama ambaye una mtoto tayari na hauhitaji mtoto kwa sasa njia
hii ni nzuri kuliko zote kwani huweza kuzuia mimba kwa miaka mitano
mfululizo kwa asilimia mia.
haiingilii utoaji wa maziwa ya mama; vidonge vya uzazi wa mpango
vyenye homoni zote mbili yaani oestrogen na progesterone kitaalamu kama
microgynon huweza kupunguza wingi wa maziwa kwani wingi wake kwenye
mfumo wa binadamu husababisha kupungua kwa homoni ya maziwa kitaalamu
kama prolactin hormone.
haiongezi uzito; inaaminika vidonge vya uzazi wa mpango huongeza
uzito kwa kuzuia kiasi kikubwa cha maji kisitoke ndani ya mwili kwa njia
ya mkojo na pia kuongeza hamu ya kula, lakini utafiti kwa wanaotumia
vijiti haujaonyesha madhara haya.
muda zaidi wa kushiriki tendo la ndoa: matumizi ya kijiti huzuia
kutoka kwa damu ya kila mwisho wa mwezi ambayo kwa wengine huambatana na
maumivu makali na kukosa raha ya kushiriki tendo la ndoa hivyo ukitumia
kijiti utapata faida hii.damu inaweza ikatoka hata mara mbili kwa mwaka
tu.
sio rahisi kwa watu wengine kujua: wasichana wengi hasa vijana
hawapendi maisha yao ya ngono yafahamike, na hasa njia hizi za uzazi wa
mpango watu wakijua unatumia wanakuona muhuni, kitu ambacho sio kweli,
hivyo matumizi ya kijiti ni siri sana na sio rahisi kwa watu wengine
kujua tofauti na vidonge ambavyo sio rahisi kuvificha.
mwisho; utafiti unaonyesha utoaji wa mimba umewanyima wanawake
wengi watoto, msanii maarufu wema sepetu ambaye kwa sasa anatafuta mtoto
kwa shida sana aliwahi kukiri kwamba aliwahi kutoa mimba zamani kidogo
na huenda anajutia maamuzi yake.hivyo kama wewe ni msichana mdogo na
hutaki kuzaa kwa sasa au wewe ni mama hutaki mtoto mwingine kwa sasa
tumia njia hii ya uzazi wa mpango.
COMMENT AND SHARE..............!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!