
Mfanyabiashara na 'motivation spekear' Eric Shingongo amefunguka na
kutoa darasa kwa baadhi ya watu ambao wamekuwa wakifanya vitu nje ya
uwezo wao ili tu kutaka kujionesha kwa watu kuwa na wao wanaweza au wana
uwezo huo.
Eric Shingongo
amewasahi watu kutunza fedha na kufanya matumizi vizuri na kile
wanachokitunza wasikae nacho tu ndani bali wanatakiwa kukiwekeza ili
kiweze kuzalisha zaidi kuliko kukaa tu ndani.
"Mimi ni mfanyabiashara, hakuna kitu
ninachokiangalia kama kubana matumizi yangu. Siwezi kununua kitu kwa
milioni tano na wakati kuna uwezekano wa kukipata kwa milioni mbili tena
kikiwa na ubora uleule. Kadri siku zinavyokwenda mbele, nabadilisha
maisha yangu, sipendi kurundika vitu vingi vya bei kubwa, labda mwingine
angeona fahari kumiliki nguo za bei mbaya, kwangu, siwezi kuishi maisha
hayo". Alisema Eric Shingongo
Shingongo anaendelea kusema kuwa hata
kama una pesa kiasi gani kumbuka kubana matumizi ya fedha na unapaswa
kufanya manunuzi kutokana na uwezo wako.
"Fanya manunuzi kutegemea na uwezo wako
usifanye mambo ili uonekane! Tunza fedha hali ni mbaya, unayoitunza
iwekeze. Ndugu yangu bana matumizi yako ya fedha na fanya manunuzi ya
kawaida hata kama una fedha kiasi gani" alisisitiza Eric Shingongo
COMMENT AND SHARE.......................!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!