
Msanii wa muziki wa Injili, Emmanuel Mbasha amesema bado anamuhitaji
aliyekuwa mke wake Flora Mbasha ingawa anadai tayari ameshazaa nje ya
ndoa na mwanaume mwingine.
Muimbaji huyo amedai ameshafanya jitihada mbalimbali bila mafanikio kwa
kipindi cha miaka miwili ili kurudiana na mama watoto wake huyo.
“Moyo wa kurudiana nilikuwa nao sana, tena sana, ikiumbukwe mambo
yametokea 2014, mwaka huo mzima nilikuwa namuomba Flora rudi nyumbani
tuendelee na maisha, 2015 nikaendelea kumuomba rudi nyumbani tuendelee
na maisha. Tumeitisha vikao vya kila aina ili kusuluishwa lakini bado
amekuwa mgumu lakini nadhani tayari alishapanga haya yatokee ndio maana
akaamua yeye kuniacha mimi nilikuwa sina mpango huo,” Emmanuel Mbasha
alikimbia kipindi cha Enewz cha EATV..
“Mimi sijaachana naye, sema tumetengana na kipindi tumetengana amepata
mtoto labda kuna kitu anaogopa, lakini mimi sina tatizo naye, Flora mimi
nakuhitaji rudi nyumbani tuendelee na maisha,” aliongeza.
Muimbaji huyo alishinda kesi ya ubakaji iliyokuwa ikimkabili baada ya Mahakama kuthibitisha muimbaji huyo hakuwa na hatia.
Kesi hiyo ilifunguliwa na mke wake huyo akimtuhumu aliyekuwa mume wake huyo kumbaka binti yatima ambaye walikuwa wanaishi naye.
COMMENT AND SHARE...............!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!