Katibu mkuu wa NNE wa umoja wa mataifa BAN KI MOON ameanga rasmi
wafanyakazi wa umoja huo baada ya kuhudumu kwa miaka kumi katika awamu
mbili za miaka mitano mitano.
Katibu mkuu wa NNE wa umoja wa mataifa BAN KI MOON ameanga rasmi
wafanyakazi wa umoja huo baada ya kuhudumu kwa miaka kumi katika awamu
mbili za miaka mitano mitano.
BAN amesema yeye hatokuwa tena Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
lakini atakuwa Balozi mwema na kwamba ilikuwa ni fahari kwake kuongoza
shirika ambalo limejitahidi kupunguza migogoro ya kimataifa na kukomesha
mateso lengo alilotimiza kwa kushirikiana na wenzake.
BAN ambaye ni raia wa KOREA KUSINI alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa
Umoja wa Mataifa mwaka 2006 na kuanza rasmi kazi tarehe Mosi Januari
mwaka 2007, jukumu ambalo amemaliza leo tarehe 31Desemba 2016.
Kuanzia kesho Jumapili waziri mkuu wa azamani wa URENO, ANTONIO
GUTERRES, mwenye umri wa miaka 67, atachukuwa wadhifa wa katibu mkuu wa
umoja huo. GUTERRES ndiye kiongozi wa kwanza wa zamani wa serikali,
kuongoza Umoja wa Mataifa.
COMMENT AND SHARE...................!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!