Mashindano makubwa ya Tennis yaani Gland Slam ya AUSTRALIAN OPEN
yanaanza kutimua vumbi hapo leo Jumatatu kwenye mjii wa MELBOURNE
nchini AUSTRALIA.
Katika siku hiyo ya kwanza ya mashindano hayo itashuhudia
mcheza Tennis namba moja kwa ubora kwa upande wanaume SIR ANDY MURRAY
akishuka dimbani katika harakati zake za kuwania taji la Gland slam ya
kwanza kwa mwaka huu, siku ambayo pia nyota ROGER FEDERER na STAN
WAWRINKA nao watashuka dimbani.
Bingwa mtetezi na mchezaji namba mbili kwa ubora kwa wanaume NOVAK
DJOKOVIC, yeye atashuka dimba kesho jumanne kucheza na FERNANDO VERDASCO
wa HISPANIA na STAN WAWRINKA atacheza na MARTIN KLIZAN wa SLOVAKIA
kesho jumatatu.
Kwa upande wa wanawake bingwa mtetezi ANGELIQUE KERBER wa Ujerumani
atacheza LESIA TSURENKO na SERENA WILLIAMS yeye ataanza harakati zake
za kuwania taji la saba la mashindano hayo ya AUSTRALIA OPEN kwa kucheza
na BELINDA BENCIC wa USWISI.
COMMENT AND SHARE..................!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!