MKAZI wa Kijiji cha Kimelembe wilayani Ludewa, mkoani Njombe, Maria
Kayombo (31) amenusurika kifo baada ya kunywa maji ya betri kutokana na
wivu wa kimapenzi.
Akizungumza na MTANZANIA jana, mama mzazi wa mwanamke huyo Magdalena
Kayombo alisema tukio hilo lilitokea juzi ambapo alipigiwa simu akiwa
shambani kuwa hali ya mtoto wake ni mbaya baada ya kunywa sumu.
Alisema walimkimbiza katika zahanati ya jirani ambapo alipatiwa
matibabu na kumweleza kuwa alikuwa amekunywa maji ya betri baada ya
kugombana na mumewe, Peter Henjewele akimtuhumua kuwa na ‘mchepuko’.
“Sikuweza kumhoji sana kwani nilishikwa na mshangao aliponiambia
amekunywa maji ya betri ili afe amuache mumewe aendelee kuwa na
mchepuko,” alisema.
Akizungumzia hali hiyo baada ya kupata nafuu mwanamke huyo alisema
chanzo cha yeye kuchukua uamuzi huo ni kitendo cha mume wake kuwa na
wanawake wengine nje.
“Tulianza nae maisha katika hali ngumu, kitendo cha kuanza kuchepuka
wazi wazi na wanawake wengine ni dharau nikaona bora nife kuliko
kuvumilia maumivu hayo ya kimapenzi,” alisema.
Hata hivyo, mume wa mwanamke huyo, alitokomea kusikojulikana baada ya kuona mke wake amekunywa maji ya betri.
PATA APP YAKO HAPA(GET YOUR APP HERE)
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!