Ili mapenzi yaweze kuwa bora kwa kila aliye katika mahusiano, huwa ni
vyema kila mmoja kuiona thamani ya mwenzake. Ukipenda kujiangalia
mwenyewe si ajabu mwenzako kupata hisia za kuwa humthamini wala
humjali.
Muunganiko wenu katika mapenzi maana yake tayari mmekuwa kitu kimoja. Katika mimi unaweka sisi.
Ila pia ni vyema ikakumbukwa ladha na maana halisi ya mapenzi ipo kwa
anayekupenda na kukuthamini. Unapokuwa na uhakika kama anakupenda na
kukuthamini hapo ndipo nafsi yako itatulia na kuwa na amani. Ndani ya
mapenzi na mtu wa aina hii ni amani na utulivu kwa kwenda mbele. Hakuna
majuto wala majonzi ya kila siku.
Unapoamua kuwa katika mahusiano na mtu ambaye hakupendi, bali unakuwa
naye kwa kuwa tu unampenda jua umejiingiza katika utumwa. Mapenzi ni
suala la kihisia zaidi. Mwenzako anapokosa hisia na wewe maana yake hata
uwepo wako hauthamini inavyopaswa. Na hapo ndiyo tunaona yale mahusiano
ya kingono yanapozaliwa na si ya kimapenzi kwa maana halisi.
Yaani mwenzako anapokuwa na mihemko ya kingono ndipo anapokutafuta na
si vinginevyo. Niliwahi kuongea na msichana mmoja aliyewahi kuniambia
anampenda kijana mmoja ambaye anauhakika kabisa yeye hampendi. Alinambia
uhakika huo kaupata kutokana na kijana huyo kumtakia kuna msichana
yupo anampenda na kumjali ila si yeye.
Kuonesha zaidi kumpenda msichana yule mwingine, jamaa aliwahi
kumwambia kama ikitokea hata huyu msichana akagombana na yule mpenzi
mwingine wa yule jamaa, kijana yule alikuwa radhi kumdhuru huyu
msichana.
Hata kwa matazamo wa haraka hapo unaweza kugundua ni kwa namna gani
huyu msichana alikuwa haitajiki. Ila cha kushangaza msichana
huyu(aliyeongea na mimi) alimwambia mvulana husika yuko radhi kuwa naye
hivyo hivyo.
Aliamua kuwa hivyo akiamini ipo siku jamaa atamuelewa. Kweli walikuwa pamoja. Ila unajua kinachomkuta sasa?
Kila jamaa anapogombana na yule msichana mwingine anamtumia huyu
kingono na mambo mengine yasiyo ya kimapenzi, na bila kutafakari mara
mbili huyu msichana anafanya kwa kile anachoamini hali hiyo itamfanya
huyu jamaa amfikirie zaidi. Kuna kitu cha kuangalia hapa.
Suala la mapenzi si suala la kuoneana huruma wala aibu. Mapenzi ni
hisia. Unapojitoa kwa mwenzako kwa kila jambo na unamuona haelekei ujue
hana hisia na wewe. Kwanini unakubali kuteseka na kuumia kila siku kwa
kumuangalia yeye tu?
Ndiyo, unampenda sana, unamjali sana na unamuhitaji sana, ila kama
yeye hakutaki wa kazi gani? Ni muda wa kujiangalia na wewe sasa.
Ona thamani yako kama binaadamu, jionee huruma jinsi unavyoteseka kila siku kwa mtu asiyeona thamani yako.
Wewe ni binaadamu mwenye hadhi na thamani, bila kujali muonekano wala
rangi yako. Unahitaji mwenye kukuthamini na kukujali na si anayekufanya
kama mdoli wake ngono au kadi yake ya pesa. Kataa utumwa wa mapenzi kwa
kuiona thamani yako.
Ni vyema ukalia kwa kumkosa kuliko kuonekana unaye wakati moyoni siyo
wako. Hakuna sifa ya kuwa na mtu mwenye fedha au muonekano mzuri ikiwa
hakujali wala haupo moyoni mwake. Mapenzi ni amani na raha.
Mapenzi hufanya watu wafurahi na kusahau shida zao. Ila jiulize
kwanini kwako hayako hivi? Unaenda kwa mwenzako badala afurahie uwepo
wako, yeye anaona unajipendekeza. Unampigia simu na kumpa maneno mazuri
ya faraja, yeye anaona unamsumbua. Sasa wa kazi gani? Siku njema
wapendwa.
COMMENT AND SHARE......................!!!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!