AMBO ya kuzingatia kabla ya kujiingiza katika mahusiano ya kimapenzi:;
on
Get link
Facebook
X
Pinterest
Email
Other Apps
Mapenzi ni moja ya mahitaji muhimu ya wanadamu, kila mmoja wetu
ahahitaji kupenda na kupendwa, hapo hamna majadiliano ndio jinsi
tulivyoumbwa. Katika enzi za mababu zetu, watu walikuwa wanaishi kwa
raha, amani na upendo japokuwa walikuwa wanachagulia wake au waume wa
kuishi pamoja kama mke na mume, enzi hizo zimepitwa na wakati siku hizi
watu wanajitafutia wenza wao wenyewe, ila siku hizi watu ndio hawana
amani, ndoa zinavunjika kila siku na wanaobakia kuteseka zaidi ni watoto
ambao wanaishia kuishi bila mama na baba.
Ukweli ni kwamba inachukua muda mrefu kumfahamu mtu vizuri, kikubwa
zaidi watu wanabadilika jinsi wanavyokuwa, hela zinaongezeka au kupungua
na wanajikuta wanavutiwa na watu wa aina tofauti. Kwa wale ambao
hawajabahatika kupata wenza wao kuna mambo ya msingi ya kuzingatia kabla
hujajizamisha katika dimbwi la mapenzi, ukizingatia mambo haya, hata
kama mtu uliyenaye atabadilika , uwezekano wa kuvumiliana na kuweza
kuishi pamoja ni mkubwa zaidi.
1. ni lengo (ambition),
kama mmoja kati wa wapenzi (nazungumzia wapenzi ambao wanampango wa
kuishi pamoja kama mke na mume) ni mtu wa kuwa na malengo na anataka
kufanya kitu fulani au kuwa mtu fulani katika maisha yake na mwenzake
anachukulia siku kama inavyokuja (laid back), huyu ambaye ana malengo
atamchukulia ambaye ni “laid back” kama ni mvivu. Wapenzi wanatakiwa
wasipishane sana katika malengo yao hata kama wana kazi mbali mbali.
2. ni uwazi (openness),
kama mpenzi wako ni “open minded” anapenda kujifunza vitu tofauti,
kujaribu vyakula tofauti, kusafiri n.k. Yule ambaye anapenda kujifunza
mambo mapya kila siku atamuona mwenzake anaboa.
3. wapenzi wanaweza kuwa tofauti katika ujuzi wa hisia (emotional intelligence).
Hapa kama tofauti sio kubwa, watu wanaweza kuvumiliana na kuishi pamoja,
ila kama tofauti ni kubwa sana, yule ambaye hana ujuzi wa hisia,
atakuwa anamburuza na kumharibia mudi yule ambaye amesimama imara kwenye
mambo ya hisia. Onyo kwa wanaume ambao wana ujuzi au utaalam wa kusoma
hisia za wanawake, wanawake ambao wana F katika ujuzi wa hisia huwa
wanavutiwa sana na watu kama ninyi.
4. ni usosho,
kama mmoja wenu ni mtu wa watu anapenda kuongea na watu na anamarafiki
kibao, utamkwaza ambae ni mtu ambaye anapenda maisha “private” na ya
utulivu. Mwenzako atakuwa bize anaweka picha zenu na status zinazowahusu
facebook wakati wewe unataka mambo ya ndani yawe ya ndani tu. Kama
tofauti si kubwa sana mnaweza vumiliana kama tofauti ni kubwa, muda si
mrefu mtashindwana
5. ni wivu.
Wivu ni kitu kibaya sana, kama mpenzi mmoja ana wivu ni ngumu kuekewana
na ambaye hana wivu. Kama wote mna wivu, sawa kwani kila mmoja ataepuka
kufanya mambo ambayo yanamuumiza mwenzake, ila kama mmoja ndio ana wivu
ataona mwenzake hajali, basi ukimuona mwenzako anaongea na classmate
wake wa zamani au ukiona mtu amepiga picha na mpenzi wako ameshikwa bega
basi inakuwa fujo tupu. Kama upo tayari kwenye uhusiano, na mwenzako
ana wivu, jaribu kumuelewesha kwamba kum-kumbatia rafiki yako sio kwamba
ndio una mipango mingine ya siri.
Kikubwa katika yote ni uaminifu, kama hamna uaminifu katika mapenzi au
ndoa. Usipasue kichwa, ondoka na tafuta mtu ambaye anakuamini au kama
haupo tayari kuwa mwaminifu usijiingize katika mahusiano, utajiumiza
mwenyewe na mwenzako. Msome mwenzako kabla ya kuanza kuitana wachumba,
kama tangu siku ya kwanza mwenzako ana wasiwasi na wewe ukikaribia simu
yake, ni afadhali umuulize mapema, kulikoni? Kama umepoteza uaminifu
katika mahusiano yako, usihofu, muonyeshe mweza wako kwamba umebadilika
na jinsi muda unavyoenda atajifunza kukuamini tena.
Hizi sifa zilizotajwa hapo juu sio za kina sana, lakini ni moja wapo ya
mambo ya kuzingatia katika kuchagua mwenza wako wa maisha(kama basi
mapenzi yana macho) kabla ya kujizamisha katika mapenzi. Je wewe unaona
ni mambo gani ya kuzingatia katika mahusiano na ni mambo gani
yanasababisha ndoa kuvunjika? Usisite kuandika maoni yako.
COMMENT AND SHARE.................!!!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!