Vyombo vya habari nchini Marekani
vimesema kuwa aliyekuwa rais wa taifa hilo George Bush anapata matibabu
katika hispitali moja ya Houston katika jimbo la texas.
Maelezo
kuhusu hali yake hayajatolewa ,lakini mkuu wa wafanyikazi wake
amenukuliwa akisema kuwa bw Bush aliye na umri wa miaka 92 yuko katika
hali nzuri na kwamba huenda akatolewa na kwenda nyumbani katika siku
chache zijazo.
Bush kama marais wengine wa zamani anatarajiwa
kuhudhuria kuapishwa kwa rais mteule wa Marekani Donald Trump katika
sherehe itakayofanyika siku ya Ijumaa.
COMMENT AND SHARE.................!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!