Maelfu ya raia wa Taiwan kutoka
makundi yaliyo na misimamo tofauti wanaandamana nje ya bunge la taifa
hilo wakati ambapo kamati ya bunge inatathmini mapendekezo ya
kuhalalisha mapenzi ya jinsia moja.
Waandamanaji wanaopinga mswada
huo wa sheria wanapiga kelele wakisema 'ndoa yafaa kuamuliwa na kila
mtu', 'andaeni kura ya maoni'.
Kulitokea mfarakano baina ya
polisi na waandamanaji, waliokuwa na nia ya kuingia ndani ya bunge
kusambaratisha shughuli za kamati ya bunge inayotathmini mswada huo wa
sheria.
Wapinzani, wengi wakitoka kwenye makundi ya kidini
wanasema kuhalalisha ndoa za jinsia moja kutasambaratisha msingi wa
familia, shule zitaanza kutoa mafunzo ya jinsia moja, na pia wanafunzi
huenda wakajaribu kuwa wapenzi wa jinsia moja.
Iwapo sheria hiyo itapitishwa, Taiwan itakuwa taifa la kwanza bara Asia kuidhinisha ndoa za wapenzi wa jinsia moja.
Mirengo yote ya kisiasa inaunga mkono sheria hiyo, japo kura ya maoni imebaini kwamba raia wanatofautiana kimawazo.
COMMENT AND SHARE...........!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!