Wakimbizi vijana wakamatwa Ujerumani kwa kutaka kuua
on
Get link
Facebook
X
Pinterest
Email
Other Apps
Mamlaka nchini Ujerumani
imewafungulia mashtaka vijana saba wakimbizi kwa jaribio la kutaka
kumuua mtu asiye na makazi kwa kumchoma moto, wakati wa sikukuu ya
Krisimas.
Washukiwa sita ambao wana kati ya miaka 15 na 18,
walijisalimisha wenyewe baada ya polisi kuonesha picha zilizorekodiwa
katika kamera ya uchunguzi, kuhusiana na shambulio hilo lililofanywa
katika treni za chini ya ardhi mjini Berlin.
Hata hivyo mtu huyo hakudhurika.
Mshukiwa
wa saba wa shambulio hilo, mwenye umri wa miaka 21, ambao polisi
wanadai kuwa ndio mshukiwa mkuu, alikamatwa karibu na nyumbani kwake.
Watuhumiwa sita kati ya hao wanatokea Syria, huku mmoja akitokea Libya.
Wote hao walikwenda Berlin Ujerumani kama watu wanaotafuta makaazi mwaka 2014 na 2015.
COMENT AND SHARE..........!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!