
Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump, ametangaza kuvunjilia mbali
shirika lake la utoaji misaada, ili kuzuia aina yoyote ya muingiliano wa
kikazi wakati akiwa Rais. Bwana Trump amesema shirika hilo limetoa
msaada mkubwa wa mamilioni ya dola, ili kufadhili miradi mbalimbali,
lakini sasa ameachana nalo kwa manufaa ya cheo chake mpya kama Rais wa
Marekani. Mwanasheria mkuu wa New York, amekuwa akichunguza wakfu huo
wa kibinafsi wa Bwana Trump, ikiwa unafuata kila kanuni ya sheria
zinazolinda mashirika ya misaada na mchango kwa makundi mbalimbali ya
kisiasa, na mwezi Oktoba mwaka huu, aliamuru ikome kukusanya fedha.
COMMENT AND SHARE...........................!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!