Kiwango cha homoni huongezeka sana mwanamke akiwa na mimba
Wanasayansi wanasema kuwa mjamzito hubadilisha ubongo wa mwanamke, kwa kipindi cha hadi miaka miwili.
Wanasema
uja uzito hupunguza seli za ubongo katika baadhi ya sehemu za ubongo wa
mwanamke, ili kumuwezesha kuhusiana vyema zaidi na mtoto na kujiandaa
kwa majukumu yake kama mama.
Uchunguzi ulifanyiwa wanawake 25
waliokuwa wameshika mimba kwa mara ya kwanza ulionyesha mabadiliko hayo
kwenye ubongo hudumu kwa hadi miaka miwili baada ya mwanamke kujifungua.
Watafti hao wanasema vipimo vya sehemu tofauti za ubongo hubadilika kipindi hicho, sawa na inavyofanyika mtu anapovunja ungo.
Lakini hata hivyo, hawakupata ushahidi wowote wa kuathirika kwa uwezo wa mwanamke kuweka kumbukumbu.
Wanawake wengi husema huwa wanajihisi kuwa wasahaulivu na kuwa wepesi wa kuekwa na hisia wakati wanabeba mimba.
Mara nyingi huwa wanalaumu kilichobandikwa kuwa ubongo wa "uja uzito" au "mtoto".
Ongezeko la homoni
Mwanamke anapokuwa na mimba, kiwango cha homoni ya oestrogen huongezekana sana na pia mwili wake kubadilika, watafiti wanasema.
Hata hivyo, si wataalamu wengi walikuwa wamechunguza mabadiliko kwenye ubongo.
Watafiti kutoka vyuo vikuu vya Universitat Autonoma de Barcelona na
Leiden walichunguza ubongo wa wanawake kabla ya kushika mimba, muda
mfupi baada ya kujifungua na miaka miwili baadaye kuangalia mabadiliko
kwenye ubongo.
Matokeo ya utafiti wao yamechapishwa kwenye jarida la Nature Neuroscience.
Mabadiliko hayo kwenye ubongo yanaaminika kuwaandaa wanawake kuwa na uhusiano mwema na watoto wao
Walilinganisha mabadiliko hao kwenye ubongo wa wanawake na ubongo wa
wanaume 19 waliokuwa wamekuwa baba mara ya kwanza,wanaume 17 ambao
hawakuwa na watoto na wanawake 20 ambao hawajawahi kujaliwa watoto.
Walishuhudia kupungua sana kwa seli za ubongo katika maeneo ambayo hutumiwa na ubongo katika kuhusiana na watu wengine.
Watafiti
wanasema mabadiliko hayo huenda ni ya kuwafaa wanawake kwa njia kadhaa
zikiwemo - kuwawezesha kupangia mahitaji ya watoto wao, kuwa na ufahamu
zaidi kuhusu hatari kwa watoto wao kutoka kwa jamii na pia kuwawezesha
kuhusiana zaidi na watoto wao.
COMMENT AND SHARE........................!!!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!