Donald Trump ameitaka Marekani kuboresha zaidi uwezo wake wa zana za nuklia.
Rais
huyo mteule ambaye ataingia ofisini mwezi ujao amesema kuwa Marakani ni
lazima ichukue hatua kama hizo, hadi wakati ulimwengu utatathmini suala
la nuklia.
Trump aliyazungumza hayo saa kaadha baada ya rais wa
Urusi Vladimir Putin kusema kuwa Urusi inahitaji kuboresha uwezo wake
silaha za nuklia.
Marekania ina silaha 7,100 za nuklia huku Urusi ikiwa inamiliki
silaha 7,300 kulingana na shirika la kudhibithi silaha la marekani.
Trump aliyaandika hayo kwenye akaunti yake ya mtando wa twitter
Wakati wa kampeni, Trump alisema kuwa silaha la nuklia ndilo tatizo kubwa zaidi linaloikumba dunia.
Mgombea
wa chama cha Democratic Hillary Clinton mara kwa mara alimtaja Trump
kuwa mtu asiye na uvumilivu wa kuweza kuzuia vita vya kinuklia.
COMMENT AND SHARE......................!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!