Tamko la Zitto Kabwe kuhusu madeni anayodaiwa, mshahara na mali alizonazo:;
on
Get link
Facebook
X
Pinterest
Email
Other Apps
Leo
December 30, 2016 Mbunge Zitto Kabwe kutoka Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo)
kupitia akaunti yake facebook ametoa taarifa kuhusu madeni anayodaiwa,
kiwango cha mshahara wake wa mwaka, kiasi cha pesa kilichopo benki,
posho pamoja na mali zote anazomiliki.
Hiki kimeandikwa na Zitto Kabwe leo.
Ndugu
Watanzania, Kama mnavyofahamu kuwa ibara ya 132(4) na (5) na Sheria ya
Maadili ya Viongozi wa Umma, Sheria namba 13 ya mwaka 1995 inataka
viongozi wote wa umma kujaza fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni.
Tamko hilo huwasilishwa Sekretariat ya Maadili ya Viongozi kabla ya
mwisho wa kila mwaka. Kama nifanyavyo siku zote, nawajulisha rasmi
kwamba nimetimiza matakwa hayo ya katiba na sheria kuhusu Maadili ya
Viongozi.
Inafahamika
kuwa Chama Cha ACT Wazalendo, kwa mujibu wa Katiba yake na Azimio la
Tabora, kimeelekeza kuwa Viongozi wake wote waweke wazi kwa Umma Tamko
la Mali, Madeni na Maslahi. Kwa kufuata masharti ya Katiba ya Chama Cha
ACT Wazalendo natangaza rasmi fomu zangu nilizowasilisha Leo Sekretariat
ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
Ni
matumaini yangu kwamba itafikia wakati Daftari la Rasilimali na Madeni
la Viongozi wa Umma litakuwa linawekwa wazi kwa Umma ili wananchi waweze
kujua Mali, Madeni na Maslahi ya Viongozi wao na pale ambapo kiongozi
ametoa habari zisizo sahihi au kuficha mwananchi aweze kutoa Taarifa
kwenye Sekretariat na Baraza la Maadili liweze kufanya kazi yake
ipsavyo.
Mfumo wa
kuweka wazi Rasilimali na Madeni ya Viongozi wa Umma ni mfumo endelevu
na muhimu kwenye vita vita dhidi ya ubadhirifu na ufisadi. Mataifa
kadhaa duniani hutumia mfumo huu ( public disclosure of leaders’ assets
and liabilities) kuwezesha mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi. Nchini
Uingereza na Kanada kwa mfano, daftari la matamko ya Rasilimali na
Madeni ya Viongozi lipo wazi kwa kila mwananchi kuona na huuzwa kwenye
duka la vitabu la Bunge.
Namsihi
Sana Rais John Pombe Magufuli kusaidia kufanya mabadiliko makubwa ya
Sheria ya maadili ya Viongozi ili kurejesha na kuboresha Miiko ya
Viongozi katika kuimarisha vita dhidi ya ufisadi nchini. Rais aliahidi
kuweka wazi Mshahara wake alipokuwa anazungumza katika kipindi cha 360
cha Clouds TV. Ninamkumbusha afanye hivyo na pia aweke wazi Mali, Madeni
na Maslahi yake ya Kibiashara ili awe mfano kwa Viongozi wengine
Nchini.
Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto, Mb
Kigoma Mjini
30/12/2016
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!