
Taasisi moja isiyo ya kiserikali ya GIRL GUIDE, imeiomba serikali
kukagua maeneo ya kufanyia biashara ya kuuza vileo katika maeneo ya
makaazi ya watu kabla ya kutoa lesini za biashara hiyo ili kuthibiti
unywaji wa vileo kwa watoto.
Taasisi moja isiyo ya kiserikali ya GIRL GUIDE, imeiomba serikali
kukagua maeneo ya kufanyia biashara ya kuuza vileo katika maeneo ya
makaazi ya watu kabla ya kutoa lesini za biashara hiyo ili kuthibiti
unywaji wa vileo kwa watoto.
Akizungumza kwenye mdahalo uliowahusisha wanafunzi kutoka shule
mbalimbali jijini DAR ES SALAAM, Katibu wa shirika hilo GRACE SHABA
amesema utoaji wa leseni bila ukaguzi unasababisha biashara ya uuzaji wa
vileo kufanyika katika mazingira hatarishi kwa watoto kujihusisha na
matumizi ya vileo na kusababisha madhara mbalimbali.
Kwa upande wake Afisa Elimu Wilaya ya KINONDONI, MARIETHA KAYOMBO
amewataka wazazi kushirikiana na walimu katika kusimamia makuzi ya mtoto
ili kumlinda na mazingira hatarishi ikiwemo uvutaji wa madawa ya
kulevya na unywaji wa vileo.
Nao wanafunzi walioshiriki mdahalo huo wametoa wito kwa wanafunzi
wenzao kusoma kwa bidii ili kujiepusha na mazingira hatarishi ikiwemo ya
matumizi ya vileo.
COMMENT AND SHARE..................................!!!!!!!!!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!