Roboti inayoweza kushiriki ngono na binadamu huenda ikazinduliwa mwaka ujao
Je ungependelea kushiriki ngono na roboti? ungefunga ndoa na roboti? na Je roboti anaweza kuwa na haki ya kupinga ndoa hiyo?
Haya
ni baadhi ya maswala machache yanayoulizwa katika mkutano wa pili wa
kuwa na mpenzi wa roboti mbali na kushiriki naye ngono katika chuo kikuu
cha Goldsmith mjini London baada ya serikali ya Malaysia ambayo ndio
iliokuwa taifa la maandalizi ya mkutano huo kuupiga marufuku.
Hatua hiyo imezua utata sio tu kwa mataifa yenye maoni ya Kihafidhina .
Hakukuwepo na wawakilishi kutoka kwa sekta ya ngono wala roboti za ngono katika mkutano huo.
Kampuni ya Real Dolls inayotengeza wanaserere wa ngono ilidai kwamba
itatengeza roboti wa ngono aliye na akili bandia mwaka ujao.
Uzinduzi
huo iwapo utafanyika utakuwa ushahidi wa David Levy ambaye amekuwa
akitabiri ujio wa roboti zinazofanana na binadamu zenye akili bandia.
Alitoa hotuba ya kufunga mkutano huo ambapo alipendekeza utengezaji wa roboti za ngono.
''Tuna roboti za urafiki na sasa roboti ambaye anaweza kuwa mpenzi ndio mtindo mpya''.
Kwa wengine kushiriki ngono na roboti ni ndoto yao lakini kwa wengine ni uharibifu mkubwa
Katika kipindi cha miaka 10 ijayo, inawezakana kutengeza roboti
ambayo watu wataihitaji kama mpenzi, ina upendo, inaaminika, inaheshima
na hailalamiki alisema.
Wengi watapendelea uhusiano huo wa roboti na huenda wakataka kufunga ndoa nao.
Mpango
huo wa mpenzi wa aina ya roboti huenda akazua maswali kadhaa ya
kimaadili, hususana wakati ambapo sheria italazimika kutambua roboti
kama binaadamu.
COMMENT AND SHARE..........................!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!