Takriban raia 20 wameuawa katika
mauaji ya kikatili katika jimbo la Kivu ya Kaskazini nchini Jamuhuri ya
Kidemokrasi ya Kongo, kulinga na taarifa zilizotolewa na maafisa
Jumapili.
Vifo hivi ni vya hivi karibuni katika wimbi la miaka miwili la ghasia katika jimbo hilo.
Mauji
hayo yametokea katika mji wa Eringeti, uliopo kilomita 55 kaskazini
mwa mji mkuu wa jimbo hilo wa Beni, mji ambao umekuwa ukikumbwa na
misururu ya mashambulio ambayo tayari yamesababisha vifo vya raia 700,
kulingana na afisa katika mkoa huo Amisi Kalonda, ambaye amewalaumu
waasi kutoka Uganda kwa mashambulio ya hivi karibuni.
Bwana Kalonda amesema kuwa wajumbe wa kundi la waasi la Allied
Democratic Forces (ADF), kundi lenye idadi kubwa ya Waislam wenye
itikadi kali kutoka Uganda ambao wamekuwa kwenye kanda hiyo kwa zaidi ya
miongo miwili , walivamia mji huo Jumamosi mchana.
"ADF wamevamia
tena wau wa Eringeti na maeneo yanayozingira mji huo asubuhi ,"
aliliambia shirika la habari la AFP, kutoka mji mkuu wa Kivu kusini wa
Goma.
"Jana, waliwauwa raia 10. Miili mingine ya watu kumi na
miwili ilipatikana Jumapili katika vijiji vinavyozingira mji ." alisema
Bwana Kalonda akiongeza kuwa waathiriwa waliuliwa kwa visu au panga''
Kwa miaka miwili iliyopita eneo linalozingira mji wa Beni limekuwa likikimbwa na mauaji ya kikatili
yaliyowauwa mamia ya raia, wengi wao wakichinjwa na kunyongwa hadi kufa.
Maafisa wa Kongo wamekuwa wakiwalaumu waasi wa ADF kwa mauaji hayo ,
lakini ripoti kadhaa za wataalam zimekuwa zikisema kuwa makundi
mengine, yakiwemo ya wanajeshi wa serikali yalihusika katika baadhi ya
mauaji.
Msemaji wa jeshi la Kongo Mak Hazukay amethibitisha
shambulio, akisema wanajeshi ''waliwauwa waasi wa ADF " lakini
akaongeza kuwa " idadi ya raia waliokufa ni kubwa".
Teddy Kataliki, mkuu wa shirika maarufu la kiraia katika kanda hiyo, pia alisema kuwa waliouawa ni 22.
Lakini kasisi wa kikatoliki katika eneo hilo amesema kuwa waliouawa ni
watu 27 na idadi inaweza kuongezeka zaidi " kama miili ya waliouawa
itabainika katika msitu" unaopakana na mji huo.
Wakati mauaji ya
kikatili ya Beni yalipofanyika Oktoba 2014, ADF walijibu haraka
wakishutumu makundi mauaji hayo kutekelezwa na maafisa wa Jamuhuri ya
Kidemokrasi ya Kongo na MONUSCO---Kikosi cha kulinda amani nchini DRC.
Kwa
zaidi ya miaka miwili sasa, mamlaka za kongo na Umoja wa Mataifa
zimeshindwa kuwalinda raia na ADF limesalia kuwa ndilo kundi
linalotawala, huku serikali ikisisitiza kuhusu uhusiano wa mauaji hayo
na vita vya kidini vya Jihad.
Mauaji haya yanatokea huku
mahusiano baina ya jamii ya kimataifa na DRC ukiwa mbaya kutokana na
hatua ya rais Josep Kabila kukataa kuachia mamlaka, licha ya muhula wake
kumalizika taraehe 20 Disemba.
COMMENT AND SHARE...........!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!