Ndege hiyo ilikuwa safarini ndani mwa Libya
Ndege moja ya Libya iliyoripotiwa kutekwa nyara ikiwa kwenye safari ya ndani mwa nchi imetua nchini Malta.
Ndege hiyo aina ya Airbus A320 ya shirika la ndege la serikali ya Libya, Afriqiyah, ilikuwa na abiria 118 wakati ilitekwa.
Watekaji nyara wawili waliripotiwa kutishia kuilipua ndege hiyo.
Ndege
hiyo ilikuwa safarini kutoka mji wa Sebha kusini magharibi mwa Libya
ikielekea mji mkuu Tripoli kabla ya kuelekezwa nchini Malta, kwa mujibu
wa shirika la habari la Reuters.
Karibu watu wote waliokuwa ndani ya ndege wanaripotiwa kuondoka.
Matakwa ya watu wawili waliokuwa na grunedi walioiteka nyara ndege hiyo haijulikani.
Meya
wa mji wa Sebha nchini Libya ambapo ndege hiyo ilikuwa ikitokea anasema
kuwa watekaji nyara hao wanatafuta hifadhi ya kisiasa.
Vikosi maalum vya ulinzi vilionekana uwanjani
Vikosi maalum vya ulinzi vilionekana uwanjani
Watekaji nyara wawili walitishia kuilipua ndege hiyo
COMMENT AND SHARE..............................!!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!