Hili ni fundisho kwa vijana wengi ambao wanataabika, suala la fedha
limekuwa mwiba mkubwa na chanzo kikubwa cha mahusiano na ndoa kuyumba.
Nimelazimika nije na ushauri huu ambao utawasaidia vijana wa kileo ambao
wanataabika na ndoa hususani suala la fedha.
Kinachowaumiza vijana wengi katika fedha na wenza wao ni tabia ya
wanaume kuwa wazi kwa kutoa taarifa za pato lake kamili. Jambo la uwazi
ni jema lakini muwe na kiasi kwani usipokuwa na akiba ya ‘taarifa za
kipato chako’ utakosa fusra ya kufanya miujiza pale mambo yanapokwama.
Fanya hivi. Mfano kipato chako ni shilingi milioni moja kwa mwezi,
mweleze kwamba unapokea shilingi laki 7 na hizo tatu hakikisha unaweka
katika sehemu salama ambayo hata ikitokea umekufa familia yako
itafaidika, mfano benki kila unapochukua mshahara hakikisha unaacha laki
tatu kama akiba asiyoijua. Sasa katika hii laki saba panga matumizi
pamoja na akiba ya pamoja.
Wanawake wanapenda ‘mshtuko/suprise’..so siku ya siku ukiona kanuna
unamtoa shoping lazima ataona umetenda muujiza kwa nia njema. Hapa ndipo
pale utasikia mwanamke anasema ‘mme wangu ana akili kweli’. Ikitokea
una marupurupu fulani kama safari nk hakikisha unatoa kiasi na ziada
unaweka chimbo. Hii itakupa upenyo wa kuwasaidia hata wazazi wako na
ndugu zako bila kumhusisha mara kwa mara kwani wanawake wengine
hawapendi usaidie ndugu na jamaa. Fanya mbinu hii hata kama kipato chako
ni laki tano weka hata elfu hamsini chimbo ili uweze kutenda baadhi ya
miujiza.
Wanawake wote duniani wamejaliwa karama ya kutumia hela yote ya
mmewe, yaani ukimwambia kuna hela hii yeye ataandika orodha ya mahitaji
ya familia ni kwani njema ila pesa zikiisha yeye hujitoa na kukulaumu
kwanini ulitumia pesa zote. Yaani dharura ikitokea yeye hayupo ni lako
hilo na ukishindwa kutatua hapo ndipo dharau inaanza…utasikia ‘mme wangu
hana msaada kabisa’ yaani hajali kabisa matatizo anatumia pesa zote
bila uangalifu.
Haya yote yanahitaji ustadi mkubwa na utimamu, kumbuka siku zote
mwanaume anatakiwa kuwa mtu wa mshitukizo/surprise kwa kutumia kipato
kile kile alichonacho. Yaani tunasema uwe na uwezo wa kutengeneza hela
(money creator). Ikitokea dharura unamuangalia usoni huku ukitabasamu,
unamwambia ‘mke wangu usihuzunike ngoja nifanye mpango nitatue hii
shida’.
Hii ndio mbinu tuliitumia sisi na kuweza kuishi na mama/bibi zenu bila bugdha.
Nawakilisha.
COMMENT AND SHARE.....................!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!