Welcome to VIVAX MEDIA, feel free to Comment and dont forget to Share (also please Click on the YOUTUBE, YOUTUBE, YOUTUBE button above/bellow the page).....!! Welcome to VIVAX MEDIA, feel free to Comment and dont forget to Share (also please Click on the YOUTUBE, YOUTUBE, YOUTUBE button above/bellow the page).....!! Welcome to VIVAX MEDIA, feel free to Comment., dont forget to Share (also please Click on the YOUTUBE, YOUTUBE, YOUTUBE button above/bellow the page).....!! Welcome to VIVAX MEDIA, feel free to Comment., dont forget to Share (also please Click on the YOUTUBE, YOUTUBE, YOUTUBE button above/bellow the page).....!!

Mark Zuckeberg: Nitasambaza internet katika nchi masikini dunia nzima:;.

                Mmiliki wa mtandao mkubwa wa kijamii duniani (www.facebook.com) Mark Zuckerberg amezidi kusisizia mpango wake wa kuhakikisha kuwa anatimiza malengo yake ya kusambaza internet kwa bei za chini zaidi dunia nzima. Mwenyekiti huyo wa facebook, ambaye alishaanza mipango hiyo kwa kuanzisha taasisi ya internet.org ambayo ina malengo ya kuhakikisha kwamba dunia nzima inaunganishwa na mtandao masaa yote bila kujali umbali au ubovu wa miundombinu duni katika nchi masikini.                                      Hivi karibuni Zuckerberg alitimiza malengo yake aliyojiwekea kwa mtandao wa facebook kuunganisha watu zaidi ya Bilioni moja duniani na sasa anataka kuhakikisha anatimiza hili.

Kupitia taasisi hii ya internet.org, Zuckerberg ameshanunua makampuni yanayotengeneza vifaa vya sola ikiwa na maana kwamba watatumia ndege aina ya drones zinazotumia nguvu ya jua kupaa katika kila pembe ya dunia huku zikigawa huduma ya internet kwa bei za chini sana.

Zuckerberg alisema hakuna tatizo sana kama watu wanavyoweza kufikiria ni vipi hili litawezekana. Alisema kuna minara mingi ya mitandao ya simu katika karibu kila kijiji katika nchi masikini. Kwa kutumia minara hii taasisi ya internet.org itaweza kushirikiana na watoa huduma za simu kama Tigo, Airtel na Vodafone ili watoe vifurushi vikubwa zaidi kwa gharama ya chini sana. Baada ya hapo, drones zitakazokuwa zikipaa angani zitatoa huduma ya mtandao kwa masaa 24 huku zikibadilishwa kadiri muda unavyozidi kusonga mbele.                                   Hata hivyo Bill Gates ambaye ni mmoja kati ya watu ambao Zuckerberg alisema walimfanya atamani kuwa kama wao, alimkosoa kwa kumwambia kwamba watu masikini kama hao wanahitaji mtu atakayetoa chanjo ya malaria ambayo haipo. Alisema mgonjwa wa maleria hawezi kunufaika na internet masaa 24. Lakini Zuckerberg anajibu kuwa, endapo watu hawa watapewa internet, itatengeneza ajira zaidi ya milioni 140 na kuwainua zaidi ya watu milioni 160 kutoka katika hali duni ya umasikini, hii itasaidia katika vita dhidi ya maleria kwani moja wapo kati ya vyanzo vya kusambaa kwa maleria ni kuishi katika maisha na mazingira duni.







COMMENT AND SHARE.............!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!

Comments

Facebook Twitter Youtube