Maneno ya rapa Nikki Mbish kuhusu hali ya Chid Benz:;
on
Get link
Facebook
X
Pinterest
Email
Other Apps
Leo
December 30, 2016 rapa Nikki Mbishi amefunguka kuhusu watu wanaolalamika
kuhusu hali ya rapa anayetawa kuwa mkali wa Freestyle Tanzania, Rashid
Makwilo a.k.a Chid Beenz a.k.a Chuma a.k.a Chid wa Ilala na kusema
kwamba watu wengi wanaolalamika hawajui ukweli kuhusu Chid.
Nikki
Mbish amesema tatizo la Chid Benz amekuwa hataki kusikia lolote kutoka
kwa watu wanaohitaji kumsaidia, na kila akisaidiwa kupelekewa Rehab
anatoroka, lakini pia watu wanaompiga picha wengi wao hawajui matatizo
ya Chid na wanataka kuonekana tu walikuwa naye.
Unaweza kusoma kila kitu alichokiandika hapa chini kupitia Instagram.
“Siwezi kupost hata picha yake wala video maana ni #FEDHEHA tu ila ukweli ni kwamba nafsi ya #CHID_BENZ haiko tayari kusaidiwa kuacha #NGADA. Kwanza kila ukikutana naye anataka aongee yeye tu maneno yake ya #LAWAMA na kujiona anaonewa ili hali ana #HAKI sana bila kujali hali aliyonayo kwa sasa.
Kuna waathirika wengi wa madawa ya kulevya hawajawahi hata kujaliwa kwa kupata hata msaada wa kupelekwa #REHAB
lakini Chid alishikwa mpaka na vitu Airport na yakasawazishwa.
Je,angeshikwa mtu mwingine si ndo ingekuwa n’tolee? He took it for
granted, he is ungrateful… Wasaidizi wamechoka pia. #NINI_KIFANYIKE na yeye hayuko tayari? – Nikki Mbishi
COMMENT AND SHARE..........................!!!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!