Watu wenye mafanikio makubwa
mara nyingi huwa ni watu ambao hawana
tofauti kubwa sana na wewe. Huwa ni watu walewale ambao pengine tunakuwa nao na
hata kupishana nao barabarani. Tofauti kubwa inayojitokeza kati ya watu hao na
wewe ni namna wanavyofikiri na matendo yao wanayoyatenda kila siku. Matendo yao
huwa yanaendana na mkabala na kile wanachokitaka maishani mwao na sio
vinginevyo.
Kwa kuwa huwa wanajua wanachokitaka
hujikuta ni watu wa kutenda na kuacha mambo ambayo wanahisi kwa namna yoyote
ile yanaweza kuwarudisha nyuma. Kwa kifupi hawa huwa ni watu wanaoshikilia
mambo wanayoona yanayowapa faida na mafanikio makubwa. Mambo yote ambayo ni
mzigo kwao huwa hawayabebi. Hicho ndicho kitu ambacho hata wewe unachotakiwa
kukifanya ili kufanikiwa zaidi.
Hutkiwi kung’ang’ania sana
mambo ambayo hayawezi kukupa mafanikio katika maisha yako. Ili uweze kufanikiwa
unalazimika kuyaacha mambo hayo mara moja. Mara nyingi umejikuta ukiwa ukikwama
kutokana na wewe kuzidi kuwa king’ang’anizi kwa mambo hayo. Huu ni wakati wa
kubadilika sasa. Kama ulikuwa hujui ama una kigugumizi juu ya hili, haya ndiyo
mambo unayolazimika kuyaacha mara moja ili kuweza kufanikiwa:-
1.
Acha kutegemea mafanikio ya haraka.
Mara nyingi hizi ndizo
zimekuwa ndoto nyingi za watu wengi kutaka kuona mafanikio makubwa na ya
haraka. Mafanikio yoyote huwa yanajengwa hatua kwa hatua. Tena kuna wakati huwa
ni hatua za kutambaa mithili ya mtoto mdogo. Kama utategemea mafanikio ya
haraka zaidi katika maisha yako hutayapata zaidi ya kujidanganya wewe mwenyewe.
Acha kung’angania mafanikio ya haraka, utakwama. Jiwekee malengo kisha songa
mbele.
2.
Acha kuwa mtu wa visingizio.
Hili ni jabo mojawapo ambalo
umekuwa ukiling’ang’ania mara kwa mara katika maisha yako. Umekuwa ni mtu wa
visingizio kwa kudai kuwa huwezi kufanikiwa kwa sababu hukusoma, huna mtaji ama
umetoka katika familia maskini. Kutokana na visingizio hivyo umekuwa huchukui
hatua yoyote zaidi ya kuzidi kufanya maisha yako kuwa magumu. Ili uweze
kufanikiwa, achana na kung’ang’ania visingizio kama mkombozi wako. Badala yake,
chukua hatua juu ya maisha yako.
3.
Acha kuogopa sana kushindwa.
Kushindwa ni hatua mojawapo
muhimu ya kuweza kukufikisha kwenye njia halisi ya mafanikio. Unaposhindwa
unakuwa unajifunza kutokana na makosa unayoyafanya na kisha kuendelea zaidi.
Kama utaendelea kuogopa kujaribu mambo mapya kila siku kwa sababu ya kushindwa,
tambua hutaweza kufanikisha mambo makubwa katika maisha yako. Ili uweze kufikia
mafanikio makubwa hutakiwi kuogopa kushindwa kwa namna yeyote ile. Unatakiwa
kuachana na woga huu mara moja ili kufikia mafanikio makubwa.
4.
Acha kufanya kazi kutegemea pesa.
Kama utaendelea kufanya kazi
na kuwaza pesa! Pesa Pesa!, hutaweza
kufika mbali sana. Fanya kazi kwa lengo la kujifunza na kisha baada ya hapo
pesa ndiyo ifuate. Ukiwa unafanya kazi kwa lengo la kupata pesa utajikuta
unafanya mambo yako mengi sana chini ya ufanisi. Badili fikra zako na acha
kung’ang’ania kufanya kazi kwa kutaka pesa tu. Ukitengeneza huduma iliyobora
zaidi pesa kama pesa itake isitake itakufuata tu huko ulipo.
5.
Acha kuwa Kufikiria sana makosa yaliyopita.
Kwa kuendelea kufikiri sana
makosa uliyoyafanya hiyo itakufanya uzidi kupoteza mwelekeo wa mafanikio yako.
Njia sahihi ya kufanikiwa ni kuachana na kufikiria makosa hayo. Vinginevyo
utakuwa unapoteza nguvu zako nyingi kun’gang’ania jambo ambalo haliwezi
kukufikisha kwenye mafanikio ya kweli. Hili ni jambo mojawapo ambalo unatakiwa
kuliacha mara moja ili uweze kufanikiwa.
Kwa vyovyote vile, kwa kadri
unavyozidi kun’gang’ania mambo hayo ndivyo ambavyo unajikuta unazidi kuharibu
maisha yako bila kujua. Ili kuweza kufanikiwa na kutimiza ndoto zako halisi
ulizojiwekea, unatakiwa kushika wajibu mmoja tu. Huu ni wajibu wa kuweza
kun’gang’ania mambo yatakayokusaidia na kubadili maisha yako kabisa. Kwa
kifupi, hayo ndiyo mambo unayotakiwa kuyaacha mara moaj ili uweze kufanikiwa.
COMMENT AND SHARE........................!!!!!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!