Ni
ngumu na kamwe siyo rahisi kumbadilisha mtu mwenye tabia ngumu awe
rafiki. Badiliko hili lawezekana ikiwa mhusika (mwenye tabia ngumu)
atadhamiria na kuwatayari kushughulika ili kubadilika.Kwa
hiyo kama ni ngumu au haiwezekani kumbadilisha basi jaribu kubadili
mtazamo wako na jinsi unavyoishi naye au nao, kwasababu mara nyingi wewe
ndiye unaye kwazika au kuumizwa wakati yeye (yule anayekuudhi)
anafanikiwa na anaendelea na furaha yake tu.Mawasiliano
baina yetu na watu wengine yanajumuisha jinsi tunavyowafanyia wengine
na jinsi wao wanavyotufanyia sisi (reaction and counter reaction). Kwa
kubadili jinsi sisi tunavyowatendea wengine inaweza kubadili jinsi wao
wanavyotutendea sisi. Hata kama ni kwa muda au kitambo kidogo tu. Hata
kama hali hii haibadili hali kwa kudumu ila inaweza kurahisisha
mazingira ya kuishi na mtu au watu wenye tabia ngumu.Kila
wakati lazima uwe na akili sana katika kuishi na watu wenye tabia
ngumu, kama hutoweza kujizuia, na ukaanza kuwabwatukia basi itakuwa
unaleta tatizo hasa pale ambapo mwenye tabia hii ngumu ni bosi wako. Je,
utaropoka au kutukana kama ulivyozoea?Hata
kama mtu au watu wenyetabia hii wako ndani ya familia na yamkini ni
wadogo kwako kiumri, bado kuropoka na kuwapayukia siyo suluhisho, hali
hii yaweza kukugharimu.Najua
kila mmoja wetu anajinsi anavyofanya kwa mtu au watu wenye tabia ngumu.
Wote hatuna namna moja, mmoja anaweza kuwa ni mkimya na mwenye ujasiri
hata anapoudhiwa, mwingine hupayuka na kumjibu yule anaye muudhi,
mwingine anaamua kulia tu anapoudhiwa, wako wanaozira na kuamua
kutozungumza tena na aliyewaudhi, wapo ambao husambaza habari mbaya
kuhusu huyo mwenye maudhi, wako ambao huamua kumwambia uso kwa uso jinsi
walivyo kwazika, sijui staili yako ni ipi.Ni
rahisi sana kuumizwa au kuudhiwa na maneno au matendo ya mwingine, na
mara mtu huyo anapojua kuwa unaumia yeye hupata nguvu, hii huwa ndiyo
silaha yake muhimu pale mnapopambana.Unachotakiwa
kufanya ni kuwaachia wakati wote wao wawe washindi, kamwe usitafute
kushindana nao, utaumia mwenyewe. Njia pekee ni kujitahidi kuwa mjanja
na mwenye akili kuliko yeye na pia kuwa na ushawishi katika yale
wanayotaka kuyatenda hata pasipo wao kugundua.
Je, unawajibu vipi watu hawa (How do you react?)Ni
jambo jema kuanza kujitazama jinsi unavyowatendea wengine na jinsi
tunavyoshughulika na wale wanaotukwaza. Kumbuka kuwa jinsi unavyoikabili
hali hiyo katika mazingira fulani inawezekana isiwe hivyo katika
mazingira mengine.Watu
wenye tabia ngumu na zinazotatiza mara nyingi huweka mitego ya maneno
au matendo na kwa kiasi kikubwa unaweza kunaswa na kuwaruhusu wakuchezee
jinsi watakavyo, na kati ya vitu wanavyo vipenda na kuvitamani ni
kukuona unalia na kuumia na kuchanganyikiwa. Kwahiyo fikiri kwanza kabla
hujafanya chochote mbele yao.Watu
watabia hii mara zote huwachukulia na kuwatendea watu wote sawa kwa
hiyo usifikiri kila alichosema au alichofanya kwako ni cha kibinafsi
sana na alikikusudia kwako. Angeweza kufanya au kusema hivyo hivyo hata
kwa mwingine aliye karibu naye wakati ule. Kwa kufahamu hili itakusaidia
kupunguza maumivu yanayoletwa na hisia zako kwake.Hembu
jiulize ni jinsi gani umewahi kukabiliana na mtu au watu wa jinsi hii,
na je ilikuwa ni kwa jinsi ya kuumiza au kuelemisha? Fahamu kwamba
kujibu kwa kupayuka, kutukana au kubishana haisaidii, bali kunakushusha
chini ya miguu ya yule aliye kusababishia maumivu hayo, na sasa atakuwa
anafurahia na kukuona wewe mjinga.Ni
chaguo lako, la ni jinsi gani utakabiliana na mtu au watu wa aina hii,
ingawa unaweza kuchagua njia bora itakayoweza kukusaidia kukuimarisha na
kupunguza udhaifu wako, zaidi ya kuamua kuchagua njia ambayo itakuacha
umeumia, umechoka, umekatishwa tamaa na umejeruhika moyo.Hii
haimaanishi uwe mtu wa kusema ndiyo tu kwa kila kitu na kila mtu, na
haimaanishi kuwa hutakiwi kukasirika HAPANA, hasira ni asili na haina
tatizo lolote hapa, ila tu matokeo ya hasira hiyo ndiyo yanayoweza
kuleta shida. Je ni jinsi gani unakabiliana na hasira yako na
unaionyeshaje? Kwa fujo, kupayuka kubishana, kulia, kuvunja vitu,
kunyamaza n.k.Ili Kujua jinsi watu wenye tabia ngumu wanavyokuathiri. Jiulize maswali yafuatayo:
Je, ni unataka kutawaliwa na wengine?Najua
jibu ni kwamba hakuna nayetaka kutawaliwa na mwingine, na ndiyo maana
unaweza kujikuta unabishana au kushindana na huyo anaye kukwaza.Tatizo
ni kwamba mwisho wewe ndiyo unaumia na yeye anabaki kufurahia kwa
kukushinda mfano; tazama fujo za madereva barabarani hususan wale wa
daladala.Nikweli unahasira naye, lakini je hiyo ni njia muafaka ya kumkabili? kumbuka mwishoni atakayeumia ni wewe.Fikiri
kama unatatizo la shinikizo la damu kama utakubali kuyumbishwa kihisia
na tabia mbovu za mwingine wewe ndiyo utabaki unaumia na siyo tu kama
hutoweza kufanya vile moyo wako utakavyo bali pia utaachwa ukijihisi
kuchoka, kuumizwa kwa hisia zako mwenyewe na kukatishwa tamaa na tabia
yako wewe mwenyewe.Nini Mwitikio wako pale unapoudhiwa? (Haswa na yule mwenye hasira na wewe)
- Je, unalipa hasira kwa hasira?
- Je, unajitetea na kuukimbia ukweli (being defensive)
- Au unajificha kutoroka au kumkwepa?
Njia zote hizi hapa juu siyo nzuri.Hata
kama una haki ya kukasirika, lakini bado atakayeumia unabaki kuwa ni
wewe. Na siyo tu utaumizwa na kukasirishwa kwa tabia yake mwenye
kukuudhi bali utaumizwa moyoni mwako kwa vile wewe ulivyotenda, dhamiri
itakushtaki zaidi (guilty conscious).
Je, unajizumgumziaje wewe mwenyewe, vibaya au vyema?Mfano: Ukweli mimi najichukia haswa ninapofikia kipindi cha mitihani au usaili.Hivi mimi nikoje?Hivi kwa nini nimeumbwa hivi?Kamwe mimi siwezi kufanya lolote jema!Wakati wote mimi ni mtu wa bahati mbaya tu!Wala
huhitaji kujichukia unapofikia wakati wa mitihani au usaili,
unachohitaji kufanya ni kujiandaa mwenyewe vizuri na kuwahi mapema
katika eneo la tukio.Hisia
potofu na zisizojenga ambazo tunajiwazia wenyewe mara nyingi
hutupotezea muda na mara tunapoziruhusu hutuharibia siku yetu nzima.Unafanya nini unapopingwa? (what do you do when you are criticized)Wako
watu wanaopendelea kupinga wengine katika kila kitu, hata katika vile
visivyostahili kupingwa,hakuna chochote chema kinachoweza kusemwa na
yeyote, bali yeye peke yake. Hata kama kilichosemwa kina ukweli kwa
asilimia kubwa basi mtu huyu atajitahidi walau kurekebisha hata lugha
tu, ili mradi kisipite hivihivi bila yeye kukipinga japo kidogo (hawa
ndiyo wale wenye tabia ngumu).Hali hii huwapa kufurahi na kujijengea nguvu kwa jinsi wanavyopinga wengine.Ni
kweli upinzani mwingine ni wa ukweli na unajenga lakini hapa nakazia
wale wanaopinga ili tu kujifurahisha nafsi zao na kuwafanya wale
wanaowapinga waumie mioyo.Je, unapopigwa, unajibuje?Je,
unajitetea au unajishusha na kukubali kila kinachopingwa kwa kuamini
kwamba anayekupinga yuko sawa na kwa hiyo unayameza maoni yako yote,
bila kuchambua kwa kina mapingamizi hayo.Kuna
jinsi ambavyo unaweza kumkabili au kumjibu anayekupinga na ikawa kama
umeweka petroli kwenye moto, upinzani utawaka na hata kuleta ugomvi,
lakini pia iko njia ambayo unaweza kumjibu mtu huyu na ukanyamazisha
fukuto lote.Je, una mtazamo hasi (mtazamo usiofaa) na wa kudumu katika kitu fulani?Mfano;
Labda unasema “Mambo yangu hayaendelei tangu nihamie katika nyumba hii,
au mambo yangu yanakwama tangu nimuoe au niolewe na huyu, ni matatizo
tu tangu tuoane, watoto hawa hasara tupu.” n.k.Mtazamo huu hasi, waweza kukugharimu siyo tu kukunyima raha bali pia waweza kuharibu hisia zako na za wengine pia.Ukijikuta katika hali hii ni vyema kujifahamu na kujitahidi kuelewa nini tatizo husika na jitahidi kubadilisha mtazamo wako.Tafuta
vile vitu ambavyo unaweza kuvitazama katika mtazamo chanya hata kama ni
vidogo. Tafuta kuviongelea vile unavyovipenda zaidi ya vile
usivyovipenda.Je, unazimeza hisia zako zote, nzuri na mbaya?
Je, unaona ni ngumu sana kusema “nakupenda” “umependeza” “umeniudhi” n.k. labda unaweza kusema neno moja tu na siyo lingine. Wengi
wetu tumekuzwa katika mazingira ambayo tunahofu kusema chochote ili tu
tusije tukamkwaza mtu, hata kama tunaumizwa au tunajisikia vyema kusema
kitu fulani, lakini tunajizuia.Badala
yake tunakwenda kusemea pembeni. Yamkini kunyamaza kunaweza kuwa na
faida katika baadhi ya mazingira lakini siyo hata katika kukubali vitu
visivyofaa. Hakuna ubaya wowote katika kuelezea jinsi unavyojisikia
moyoni mwako ili mradi tu unaeleza kila unachokihisi kwa hali njema na
siyo kwa hasira au shari. Katika hali hii kamwe hutowapoteza marafiki
zako, na kama kuna yeyote aliye rafiki atasumbuliwa na hili basi
usihofu, kubali tu kumpoteza kwa kuwa hakuwa wa muhimu au wa msaada sana
kwako.Hali
ya kujifanya hujaumia au hujakwazika na wakati umekwazika na unalia
ndani kwa ndani inaumiza na kufanya ujisikie vibaya sana. Inakufanya
uzidishe mazingira ya msongo wa mawazo (stress) hasa pale unapojiwazia
wewe mwenyewe zaidi ya kushughulika na wale waliokuudhi.Mtazamo
wako jinsi unavyojiona wewe mwenyewe huathirika sana, na pia waweza
kujisababishia tatizo hasa pale wale wenye tabia ngumu watakapo kugundua
kuwa huwezi kusema chochote hata ukiumizwa na hii itawafanya wakugeuze
mpira wa kuchezea.Je, wewe ni kati ya wale wanaojiamini kusema chochote wanachokifikiri bila kujali matokeo yake?Hebu
fikiria jinsi unavyojisikia pale ambapo mtu au watu wengine wangefanya
hivyo hivyo kwako. Je, unataka kuwasababishia wengine maumivu ya moyoni?
Kusema chochote kinachoshuka toka kichwani mwako kupitia kinywani mwako
bila kufikiri juu ya matokeo au athari zake kwa wale wanaokusiliza au
waliokuzunguka kunaweza kukupotezea marafiki na kuishusha hadhi yako kwa
urahisi sana.Mara
nyingi mtu wa jinsi hii huweza kujikuta akiwa pweke na anayepingana na
ulimwengu (kila mtu anamchukia). Hii ni kati ya hisia za kuhuzunisha na
kuumiza sana muda wote, lakini pia huumiza zaidi pale unapogundua kuwa
ni maumivu uliyojitakia mwenyewe. Peke yako unajikuta umetengwa na mtego
wa kihisia na kukuzamisha usipoweza kujikwamua tena.
COMMENT AND SHARE......................!!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!