Wizara ya Elimu, Sayansi,
Teknolojia na Ufundi imesema haihusiki na utoaji wa ajira za walimu
nchini, isipokuwa inachokifanya ni uhakiki wa taarifa za walimu wenye
sifa za kuajiriwa serikalini.
Akizungumza na EATV , Naibu Waziri wa Elimu, Mhandisi Stella
Manyanya amesema kuwa kwa sasa wizara hiyo inapitia taarifa (CV) za
walimu waliohitimu ngazi ya Stashada na Stashahada, na baada ya hapo
itazituma taarifa hizo katika Wizara ya Utumishi ambao ndiyo wanaohusika
na kuajiri.
Akizungumzia sababu za kuwatenga wahitimu wa ngazi ya cheti, Manyanya
amesema uhitaji mkubwa uliopo kwa sasa ni kwa walimu wa sekondari
hususani wa masomo ya Phisics, Hisabati, Chemistry na Biolojia, hivyo
inawahitaji kwa haraka zaidi walimu hao huku akisema wahitimu wengine
ambao siyo wa masomo hayo na ambao siyo kwa ajili ya kufundisha
sekondari, wasubiri utaratibu wa wizara inayohusika na utumishi.
"Siyo kwamba hatuhitaji walimu wa shule za msingi, lakini uhitaji
mkubwa tulionao kwa sasa ni walimu wa sekondari, sisi hatuajiri, sisi
tunafanya uhakiki, na sasa tunapitia CV za wahitimu waliotuma taarifa
zao, tukishajiridhisha na wale ambao taarifa zao ni sahihi na wana sifa
tunazohitaji, tunazipeleka Utumishi, hao ndiyo wataajiri, halafu majina
yatapelekwa TAMISEMI kwa ajili ya kupangiwa maeneo ya kazi" Amesema
Manyanya
Kuhusu idadi ya walimu wanaohitajika haraka, Manyanya amesema,
wanahitajika walimu wengi kuliko idadi waliyoitoa mwanzo, na kuwataka
wote waliotuma taarifa zao wawe na subira kwa kuwa mchako wa uhakiki
bado unaendelea na majina yatatangazwa muda mfupi ujao ambao hautazidi
kipindi cha miezi mitatu.
COMMENT AND SHARE..............................!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!