UONGOZI wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri, Dar es Salaam
umewakamata watu 13 wanaohusishwa kuvua shehena ya samaki 473 karibia
tani 1.3 wenye thamani ya Sh milioni 13 kwa kutumia mabomu.
Samaki hao aina ya kolekole, jodari, changu, pono, sehewa na nguru
waliingizwa sokoni hapo Desemba 16, mwaka huu na baada ya ukaguzi,
ikabainika kuingizwa kwa samaki hao, huku wahusika wakidaiwa kutoroka.
Kutokana na hali hiyo, Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles
Tizeba alimtaka Mwenyekiti wa Bodi ya soko hilo, kupitia upya mfumo wa
mapokezi, ulinzi na usimamizi ili kujiridhisha kama uko safi. Kuhusu
kukamatwa kwa watuhumiwa hao,
Meneja wa Soko hilo, Eliakim Mniko alisema jana kuwa, walikamatwa sokoni
hapo na wamefikishwa polisi kutoa maelezo na kufunguliwa kesi
itakayoanza kusikilizwa mapema mwakani.
Akiwa katika ziara sokoni hapo Desemba 19, 2016, Dk Tizeba alisema ni
aibu kwa kitendo hicho kufanyika meta chache kufika Ikulu na kwamba kama
suala la ukaguzi limewashinda, Bodi ya soko iachie jukumu hilo kwa
mamlaka nyingine ifanye kazi sokoni hapo.
Pia aliagiza wahusika wakamatwe na kuchukuliwa hatua, ikiwa ni pamoja na
kutangazwa kuwa ndio wanaoharamisha uvuvi na kulitia hasara taifa.
COMMENT AND SHARE.......................!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!