
Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ameitaka CCM iache kujidanganya
kuwa haiwezi kuondoka madarakani akiitaka iangalie alama za nyakati hasa
mabadiliko ya uongozi yanayotokea kwingineko duniani.
Hata hivyo, Lowassa ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema amesema
unahitajika muungano wa dhati wa vyama na uliopangiliwa vizuri katika
juhudi za kuiondoa CCM madarakani.
Lowassa alisema hayo alipoombwa na mwandishi wa habari hizi kutoa
tathmini ya maisha yake ya kisiasa mwaka mmoja na nusu tangu
alipojiondoa CCM na kujiunga na Chadema ambako aliteuliwa kuwa mgombea
urais wa chama hicho akiwakilisha muungano wa vyama vine – Chadema, CUF,
NCCR - Mageuzi na NLD – Iliopewa jina la Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa).
COMMENT AND SHARE...........................!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!