Rais mteule wa Marekani ameiambia Israel kukaa imara hadi pale atakapochukua mamlaka mwezi ujao.
Pia amesema kuwa Israel imekosewa heshima na kwamba hilo lazima lisitishwe.
Ni matamshi yake ya hivi karibuni katika mtandao wa kijamii wa Twitter.
Wakosoaji wamemwambia rais huyo mteule kutumia njia rasmi za kuwasiliana kuhusu maswala ya kimataifa.
Siku
ya Ijumaa, Marekani iliamua kutoshiriki katika kura ya vetoe kuhusu
uamuzi wa Umoja wa Mataifa unaokataza Israel kuendeleza ujenzi wa
makaazi katika maeneo ya Palestina inayokalia. Makaazi ya wayahudi katika maeneo yanayokaliwa na Israel nchini Palestina
Katika machapisho ya mtandao wa Twitter siku ya Jumatano mjini New
York, Bw Trump alisema: Hatuwezi kuruhusu Israel kutoheshimiwa.Marekani
ilikuwa rafiki mkubwa wa Israel ,lakini sio tena. Mwanzo wa kumalizika
kwa urafiki huo ni pale Marekani ilipokubali kuingia katika makubaliano
na Iran, na sasa Umoja wa Mataifa ! Kaa imara Israel,tarehe 20 mwezi
Januari inakaribia!
Zaidi ya Wayahudi 500,000 wanaishi katika
makao 140 yaliojengwa na Israel tangu uvamizi wake 1967 ambapo walikalia
maeneo ya West Bank na mashariki mwa Jerusalem.
Makaazi hayo sio halali kulingana na sheria ya kimataifa ,ijapokuwa Israel inapinga hilo.
COMMENT AND SHARE..........!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!